Esther Musila alalamika kuhusu hamu kubwa ya chakula ya mumewe, Guardian Angel

"Oneni vile bwanangu anajipenda, ebu oneni," Musila alisema.

Muhtasari

•Mama huyo wa watoto watatu wakubwa alimwonyesha Guardian Angel akiwa ameshika sahani iliyojaa chakula.

•Mwezi jana, wawili hao waliadhimisha miaka mitatu tangu walipokutana kwa mara ya kwanza.

Esther Musila na mume wake Guardian Angel
Image: INSTAGRAM// ESTHER MUSILA

Siku ya Jumanne, Bi Esther Musila alichapisha video yake akimdhihaki mume wake Guardian Angel kwa 'kuwa na pupa kubwa ya chakula’.

Kwenye Instastori zake, mama huyo wa watoto watatu wakubwa alimwonyesha Guardian Angel akiwa ameshika sahani iliyojaa chakula.

"Oneni vile bwanangu anajipenda, ebu oneni," alisema huku akionyesha sahani ambayo msanii huyo alikuwa ameshika.

Bi Musila ambaye alionekana wazi kushangazwa sana na wingi wa chakula ambacho mwimbaji huyo wa nyimbo za injili alikuwa ametia kwenye sahani yake aliendelea kumsihi wakule pamoja.

"Hii  chakula yote tutakula na wewe ama utakula pekee yako?" alimuuliza.

Guardian Angel alitikisa kichwa chake kukataa, akaondoka karibu mkewe na kuketi mbali ili kufurahia chakula hicho pekee yake.

Kwenye video, wanandoa hao waliendelea na mazungumzo yao na walionekana wenye furaha kubwa pamoja.

Mwezi jana, wawili hao waliadhimisha miaka mitatu tangu walipokutana kwa mara ya kwanza.

Esther Musila alisema wimbo wa mwimbaji huyo wa injili, 'Rada' ulikuwa mwanzo wa muungano wao wa kudumu. Alipata hamu ya kukutana na Guardian Angel baada ya kuusikia wimbo huo kwenye redio na kuupenda.

"Muungano wetu usingetokea kwa namna nyingine. Tulikuwa na mipango yetu lakini Mungu alitangulia mbele yetu na ameendelea kutuongoza katika safari yetu," Musila alisema mnamo Machi 13.

Mama huyo wa watoto watatu wakubwa alidokeza kwamba baada ya kukutana Guardian Angel kwa mara ya kwanza hakufikiria kwamba wangekuwa maestherrafiki wakubwa na hatimaye kuwa mume na mke.

"Ninashukuru kuwa na wewe katika maisha yangu. Heri ya siku ya ukumbusho wa urafiki mume wangu @guardanangelglobal Nakupenda. ❤❤❤," aliandika.

Guardian Angel kwa upande aliweka wazi kuwa alimpenda mwanamke huyo wa miaka 53 baada ya kukutana naye. Katika taarifa yake, Angel alisema alipomwangalia Bi Musila aliona sifa zote anazohitaji kwa mke ndani yake.

"13/3/2020 ulinitazama ukaona supastaa. Hamu yako ilikuwa kuniona nikiwa vile ulivyoniona. Nilikutazama na kuona kila nilichotaka kwa mwanamke. Miaka mitatu baadaye sisi sote tuna kile tulichotaka," alisema.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 33 alimtaja Bi Musila kuwa mke mzuri na kukiri mapenzi makubwa kwake. 

"Sikukosea na ninafurahi kwamba Mungu ametimiza kweli na ataendeleza kusudi langu katika maisha yako. Asante kwa Kuja. Nakupenda ❤❤," Musila alijibu