Wapenzi Karen Nyamu na Samidoh washerehekea kumbukumbu yao

Wazazi wenza hao walionekana wenye furaha sana pamoja.

Muhtasari

•Karen Nyamu alichapisha picha yake nzuri akiwa na mzazi huyo mwenzake kama njia ya kuadhimisha TBT.

•Samidoh alichukua screenshot ya chapisho la mzazi huyo mwenzake na kuchapisha kwenye ukurasa wake rasmi.

Samidoh na Karen Nyamu
Image: HISANI

Alhamisi, wapenzi Karen Nyamu na Samuel Muchoki almaarufu Samidoh walisherehekea kumbukumbu yao ya takriban miezi kumi iliyopita.

Wazazi wenza hao walionekana wenye furaha sana pamoja.

"Ka #TBT Juni 2022 @samidoh_muchoki," aliandika kwenye picha hiyo.

Pichani, wazazi wenza hao wawili walionekana wenye furaha sana pamoja wakiwa katika mahali pasipobainishwa.

Samidoh alichukua screenshot ya chapisho la mzazi huyo mwenzake na kuchapisha kwenye ukurasa wake rasmi.

Haya yanajiri takriban wiki moja baada ya Karen Nyamu kubadilisha picha yake ya wasifu kwenye mtandao wa Instagram na kuweka picha inayomuonyesha akiwa na staa huyo wa Mugithi na binti yao mdogo.

Seneta huyo alitumia moja ya picha  walizopigwa wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya binti yao Wairimu mwezi Februari. Wiki moja baada ya kuchukua hatua hiyo, Nyamu bado hajabadilisha picha hiyo.

Image: INSTAGRAM// SAMIDOH

Katika harusi ya Akothee mapema wiki hii, Karen alionekana akiimba, kucheza na kutangamana na wageni wengine kwa furaha tele.

Kwa wakati fulani, alisimama kwenye jukwaa, akapewa kipaza sauti na kuwatumbuiza wageni kwa wimbo. Aliimba  wimbo wa mpenzi wake Samidoh akimshirikisha Joyce Wamama, 'Wendo wi Cama' (Mapenzi ni matamu).

Wageni walifurahia kutumbuizwa na mama huyo wa watoto watatu huku Akothee na mumewe mpya wakicheza pamoja naye.

"Asante, asante sana," Karen alisema baada ya kutumbuiza.

Takriban wiki tatu zilizopita, wawili hao walikuwa miongoni mwa wageni walioalikwa kwenye karamu ya kutoa shukrani ya waziri wa Biashara Moses Kuria iliyofanyika nyumbani kwake katika kaunti ya Kiambu.

Video zilimuonyesha seneta huyo wa kuteuliwa akijivinjari na Samidoh wakati sherehe hiyo ikiendelea. Wawili hao ambao wana watoto wawili pamoja walionekana wenye furaha pamoja huku wakisherehekea.

Kwenye video moja, Nyamu alitumia wimbo wa Jay Melody 'Sawa' kueleza nguvu ya mahaba yake na mwimbaji huyo wa Mugithi.

"Na penzi letu ni kama sunna

Na ulinzi kama suma

Hata akinuna

Bado unapendeza mchumba

Mkimuona ananichuna

Msinionee huruma

Cha mtu huliwa na mtu

Kutu yake chuma," aliimba pamoja na Melody.