'Kweli ugonjwa wa akili ni kweli'- Tanasha amwambia shabiki kwa kumkejeli

"Fikiria kuandika na kujibu ujumbe wako, kweli ugonjwa wa akili ni ukweli," alisema shabiki huyo.

Muhtasari

•Naseeb Junior ni mtoto wake Diamond aliyezaliwa mwaka wa 2019.

Image: INSTAGRAM// TANASHA DONNA

Mwimbaji Tanasha Donna na aliyekuwa mpenzi wa msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz alimjibu kwa hasira  shabiki aliyemkejeli kwenye Instagram.

Hili lilijiri baada ya Donna kujibu kwenye posti ya ukurasa ya mtoto wake aliyekuwa ameandika ujumbe wa kuwatakia watu Eid Mubarak

"Eid Mubarak kutoka kwa mama na mimi," ilisoma ujumbe huo kutoka kwa ukurasa wa Naseeb Junior.

"Nakupendamwanangu, " Alijibu Tanasha Donna kwenye posti ya mtoto wake.

Baada ya hilo ,shabiki mmoja alijibu kwa kejeli huku akishambulia Tanasha Donna kwa kumwita mwendawazimu.

"Fikiria kuandika na kujibu ujumbe wako, kweli ugonjwa wa akili ni ukweli," alisema shabiki huyo.

Tanasha Donna alionekana kukerwa na ujumbe huo huku akijibu kwa hamaki na ujumbe wa kumshambulia shabiki huyo kwa maneno.

"Fikiria kukosa kazi mpaka unajibu ujinga kwa ukurasa wa mtoto  kwa sababu mama yake anamwonyesha mapenzi, kweli ugonjwa wa akili ni halisi," alijibu Donna.

Tanasha Donna na Diamond wana mtoto mmoja ambaye walimpata walipokuwa wakichumbiana na ye. Wawili hao walitengana mwanzoni mwa mwaka wa 2020 baada ya kuchumbiana kwa mwaka mmoja.

Tanasha Donna alitoa sababu ya kutengana kwao akisema Diamond alitupa jicho lake nje wakiwa kwenye mahusiano. Tanasha alidai kuwa japo kuwa ni mwislamu na anaelewa mambo ya wananawake wengi,yeye hakuwa tayari kwa mahusiano ya aina hiyo.