Diamond azidi kumpuuza mwanawe na Hamisa Mobetto, awapendelea wa Zari na Tanasha

Mwimbaji huyo alimpuuza Dylan huku akiwasherehekea Tiffah, Nillan na Naseeb Junior.

Muhtasari

•Siku ya Jumatano, bosi huyo wa WCB aliwasherehekea watoto wake wengine watatu na kumuacha nje Dylan.

•Mwaka jana, Mobetto alilalamika kwamba Diamond amemtelekeza mtoto wao na kueleza kwamba hajui sababu yake.

Diamond, Hamisa Mobetto
Image: HISANI

Staa wa  Bongo Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz ameendelea kujitenga na anayeaminika kuwa mtoto wake na mwanamitindo wa Tanzania Hamisa Mobetto, Dylan Abdul Naseeb.

Mnamo siku ya Jumatano, bosi huyo wa WCB aliwasherehekea watoto wake wengine watatu na kumuacha nje Dylan.

Kwenye Instagram, Diamond alichapisha picha za mazungumzo ya video kati yake na mwanawe na mwanamuziki wa Kenya Tanasha Donna, Naseeb Junior. Pia alionyesha picha nyingine ya mazungumzo yake na watoto wake wawili na mwanasoshalaiti wa Uganda Zari Hassan, Tiffah Dangote na Prince Nillan.

Mwimbaji huyo aliambatanisha picha hiyo na emoji za moyo, kuashiria upendo wake mkubwa kwa mbegu hizo zake. Pia alitumia wimbo wake 'My Baby' (Mtoto Wangu) kueleza upendo wake kwa mazao hayo yake.

"All I can see is your love ooh!

Moyo nafsi usiwe na wasi

Nimesha amua

You go be my baby (My baby!)

Be my honey (My baby!)

Be my sugar (My baby!)," aliimba.

Kumaanisha: ("Ninachoweza kuona ni upendo wako ooh!  Moyo nafsi usiwe na wasi, Nimeshaamua. Utakuwa mtoto wangu (Mtoto wangu!)  Kuwa asali yangu (Mtoto wangu!) Kuwa sukari yangu (Mtoto wangu!)"

Hii sio mara ya kwanza kwa staa huyo wa Bongo kuonyesha upendo mkubwa kwa watoto hao 3 na kumtenga mwanawe Hamisa Mobetto. Katika siku za nyuma, ameonyesha wazi kutojihusisha kwake na mvulana wa miaka 3.

Hamisa Mobetto ambaye amewahi kuwa na mahusiano na bosi huyo wa WCB anaaminika kuwa na mtoto wa kiume naye, Dylan Abdul Naseeb. Hata hivyo kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya wawili hao kuhusu mtoto huyo.

Mwaka jana, mwanamitindo huyo alilalamika kwamba Diamond amemtelekeza mtoto wao na kueleza kwamba hajui sababu yake.

Hii ni baada ya mzazi huyo mwenzake kutomsherehekea mvulana huyo mdogo akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

"Kusema ukweli sifahamu kwa nini nadhani hilo swali ni vizuri sana akiulizwa yeye mwenyewe binafsi mi ntakua sina majibu na mi si mtu ambaye anauliza nadhani ni maamuzi tu mtu unaamka tu asubui unaamua," alisema.

Hapo awali, Diamond amewahi kuibua wasiwasi kwamba huenda Dylan sio mtoto wake halisi.