Mwandani wa Harmonize, Mwijaku akiri upendo mkubwa kwa mamake Diamond

Mwijaku akiri upendo mkubwa kwa mamake Diamond

Muhtasari

•Mwijaku alimtambua Mama Dangote kama mama yake na kumtaka amwalike kwenye hafla ya Futari. 

•"Nakupenda mamangu! Nasubiria mualiko wa futari," aliandika.

Mwijaku na Diamond
Image: HISANI

Muigizaji wa Filamu Bongo Mwemba Burton almaarufu Mwijaku amekiri upendo mkubwa kwa mamake Diamond, Bi Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote.

Siku ya Jumatano, mchekeshaji huyo ambaye katika siku za nyuma aliwahi kumkosoa bosi huyo wa WCB waziwazi alimtambua Mama Dangote kama mama yake na kumtaka amwalike kwenye hafla ya Futari. 

"Nakupenda mamangu! Nasubiria mualiko wa futari," aliandika.

Mwijaku aliambatanisha ujumbe huo aliochapisha kwenye mtandao wa Instagram na picha nzuri ya mamake Diamond.

Hatua hiyo ilipokewa na mashabiki wengi wa Bongo kwa mshtuko mkubwa ikizingatiwa chuki ambayo muigizaji huyo amemuonyesha mwanawe Mama Dangote,  Diamond Platnumz katika siku za nyuma.

Mwaka jana, Mwijaku ambaye kawaida huegemea upande wa hasidi wake Diamond, Harmonize aliibua madai mengine dhidi ya dhidi ya bosi huyo wa WCB huku akimtetea Konde Boy kwa ubora wa kutunza mashairi ya muziki.

Akizungumza na waandishi wa habari,  alisema kwamba anatambua fika Harmonize ana ubora wa kiwango kilochotukuka katika kuandika mashairi ya muziki ila ana tatizo moja la kile alichokiita laana.

“Hakuta wasanii wanaoandika Tanzania, yaani ukimtoa Alikiba anayefuata ni Harmonize. Anajua sana kuandika mashairi yake, tatizo lake moja ni laana. Hakuna mtu aliyetembea na kuku na mayai yake akaishi salama. Huwezi kutembea na mtoto na mama wote, huwezi kufanya hivo ukafanikiwa,”  alisema.

Mwezi Novemba hata hivyo, staa huyo wa Bongo alifungia macho uhasidi alioonyeshwa na Mwijaku na kumbeba katika safari yake ya Qatar.

Wengine ambao walikuwa katika safari hiyo ni pamoja na Mama Dangote,  mpenzi wake Uncle Shamte, Esma Platnumz, Mbosso, meneja Ricardo Momo, msemaji wa Yanga S.C Haji Manara, Baba Levo, Mwijaku pamoja na mlinzi rasmi wa Diamond Onesmo Amos.