"Silalamiki!" Karen Nyamu ajibu kwa ukali kuhusu kuwa mpango wa kando wa Samidoh

Jumapili, seneta huyo alijitokeza akiwa amevalia sweta lenye jina la Samidoh.

Muhtasari

•"Lakini unaweza ukajiuliza kwa nini jamaa ambaye jina lake linaonekana kwenye sweta yako hakukuoa," Nyamu aliulizwa.

•Karen Nyamu ambaye kuwa na ujasiri mwingi ifikapo ni kujitetea alijibu , "Hahaha hatulalamiki punguza umama."

Image: HISANI

Siku ya Jumapili, seneta Karen Nyamu alichapisha picha yake akiwa amevalia sweta lenye jina la mzazi mwenzake, Samuel Muchoki almaarufu Samidoh.

Nia ya mama huyo wa watoto watatu na chapisho hilo la Instagram sio dhahiri lakini aliifanya ionekane kama chapisho la kawaida tu.

"Wale wanaomtazama wanang'aa, nyuso zao hazifunikwa kamwe na aibu ZABURI 34:5," Nyamu alisema chini ya picha aliyochapisha.

Wengi wa waliotoa maoni walionekana kuangazia zaidi ujumbe kwenye sweta ya seneta huyo wa kuteuliwa kuliko kitu kingine chochote.

Baadhi ya wanamitandao walidai kuwa alitoa chapisho hilo kama njia ya kumchokoza mke wa Samidoh huku wengine hata wakichukua hatua ya kumuuliza kwa nini aliweka picha hiyo na ikiwa alifanya hivyo kwa makusudi.

"Lakini unaweza ukajiuliza kwa nini jamaa ambaye jina lake linaonekana kwenye sweta yako hakukuoa badala ya mwanamke anayedaiwa kuolewa rasmi naye. Hukuzaliwa jana. Wewe ni mpango wa kando punguza kasheshe," shabiki mmoja alimwambia.

Karen Nyamu ambaye kuwa na ujasiri mwingi ifikapo ni kujitetea alijibu , "Hahaha hatulalamiki punguza umama."

Mtumizi mwingine wa Instagram alimwambia, "Wewe ni mchokozi saaana."

Katika jibu lake, mama huyo wa watoto watatu alionekana kushangaa ni nani ambaye alidaiwa kuchokoza.

"SMH uchokozi iko wapi hapa na nani anachokozwa," Nyamu alimuuliza shabiki huyo.

Kuna uwezekano mkubwa kwamba chapisho la seneta huyo wa kuteuliwa linaashiria  tu kuwa anajivunia baba huyo wa watoto wake wawili ambaye ni mwimbaji maarufu wa Mugithi au hata alikuwa akitangaza tu chapa yake.

Karen Nyamu amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Samidoh kwa muda mrefu na ingawa wao sio wanandoa rasmi, wawili hao wamebarikiwa na watoto wawili pamoja, mvulana mmoja na msichana mmoja.

Kwa muda mrefu, kumekuwa na mzozo unaodaiwa kuwa kati ya seneta huyo na Edday Nderitu kuhusu ni nani mke bora kwa Samidoh.

Mapema mwaka huu, Edday alimwandikia Samidoh ujumbe mrefu kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akimuonya kwamba hayuko tayari kamwe kulea watoto wao katika ndoa ya wake wengi.