Hamisa Mobetto nje, Khadija ndani! Kevin Sowax amfichua mpenziwe mpya mrembo

Ni rasmi kwamba uhusiano kati ya mwanamitindo Hamisa Mobetto na mfanyibiashara Kevin Sowax umekwisha kabisa.

Muhtasari

•Kevin alithibitisha hayo  Jumanne alipochapisha picha ya mwanamke mwingine anayeaminika kuwa mpenzi wake mpya.

•Mfanyibiashara huyo alichapisha picha ya mwanamke mwenye mwili mzuri na kumtambulisha kama "Khadija Sowax."

Kevin Sowax na aliyekuwa Mpenzi wake Hamisa Mobetto
Image: INSTAGRAM// KEVIN SOWAX

Ni rasmi kwamba uhusiano kati ya mwanamitindo maarufu wa Tanzania Hamisa Mobetto na mfanyibiashara tajiri wa Togo Kevin Sowax umekwisha kabisa.

Kevin ambaye anaendesha kampuni kubwa ya usafirishaji nchini China alithibitisha hayo siku ya Jumanne wakati alipochapisha picha ya mwanamke mwingine anayeaminika kuwa mpenzi wake mpya.

Mfanyibiashara huyo tajrii alichapisha picha ya mwanamke mwenye mwili mzuri na kumtambulisha kama "Khadija Sowax."

Hata hivyo, alificha uso wa mwanamke huyo kwa maandishi.

Image: INSTAGRAM// KEVIN SOWAX

Haya yanajiri wakati ambapo kumekuwa na utata mwingi na maswali mengi kuhusiana na uhusiano wa raia huyo wa Togo na Hamisa Mobetto. Wawili hao walifichua uhusiano wao mwaka jana na hapo awali walionekana kupendana na kufaana sana.

Mapema mwaka huu, wapenzi hao walizua tetesi za kuachana baada ya Kevin kufuta picha zote za Mobetto kwenye mitandao yake ya kijamii.

Hamisa alimtambulisha Sowax kwa walimwengu alipomzawadia gari aina ya Range Rover. Wakati huo pia alimshukuru kwa kumnunulia gari hilo la kifahari.

“Yani kuna wanaume…alafu kuna mwanaume wangu mimi hapa. Asante, mpenzi…Nataka kulia. Asante kwa kunionyesha upendo wa kweli ni nini. Umekuwa kitu bora zaidi ambacho kimewahi kunitokea."

"Nakupenda weeh, roho yangu weee. Kwako sijiwezi…ohh mai Laaaavuuuu," aliongeza.

Baadaye, Sowax alifunguka kuhusu uhusiano wake na Hamisa.

“Tangu nilipokuona, nilijua kuwa wewe ndiye. Kadiri ninavyozidi kukufahamu ndivyo hisia zangu zinavyozidi kukua. Ninashukuru kuwa na wewe katika maisha yangu na kufurahia uzoefu wa siku zijazo," alisema.

Mobetto alisema anahisi kama amempata mpenzi wa maisha.

“Kwa muda nilikuwa najiona sina imani na ndoa, kipindi hicho sikuwahi kuona mfano wowote kuwa niwe na ndoa yangu kama mtu fulani na mke wake.

Lakini sasa naona umuhimu wa ndoa ukizingatia sasa nina watoto na najua umuhimu wa mume utakuwa hivi na hivi, sasa naona mifano naona vitu mitandaoni hadi najisikia kuolewa,” alisema mwanamitindo huyo.

Mobetto alikuwa akimsifu mpenzi wake hata kabla ya kumfichua.

"Kwa mwanaume aliyenitengenezea sehemu yangu ambayo hakuvunja, Asante kwa kuutunza vyema moyo wangu bebb!! Hakuna mtu anayekupata kama mimi"