Hongera! Marioo na Paula hatimaye wamkaribisha mtoto wao duniani, wafichua jina lake

Marioo alimshukuru Mungu kwa zawadi ya mtoto na kumtakia bintiye maisha mema.

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo wa bongo alifichua kuwa mtoto wao wa kwanza ni msichana mrembo kwa jina Princess Amarah.

Image: INSTAGRAM// PAULA KAJALA

Msanii maarufu wa Bongo, Omary Mwanga almaarufu Marioo ametangaza kuzaliwa kwa mtoto wake na mwanamitindo Paula Paul Kajala.

Katika tangazo lake la siku ya Jumanne, mwanamuziki huyo alifichua kuwa mtoto wao wa kwanza ni msichana mrembo kwa jina Princess Amarah.

Marioo alimshukuru Mungu kwa zawadi ya mtoto na kumtakia maisha mema.

“Asante Mungu kwa Baraka hii ya Mtoto , tunakushukuru kwa Mtoto wetu wa Kwanza. Binti yetu mrembo @princess__amarah, Mungu Akukuze akujaalie Afya na Baraka Tele 🙏🏾,” Marioo alisema.

Aliambatanisha kauli yake na video nzuri ya chumba alichojifungua Paula Kajala binti yao.

“ASANTE MALKIA WANGU❤️ @therealpaulahkajala UNASTAHILI KILA KILICHOPO NDANI YA UWEZO WANGU , MUNGU AKUBARIKI SANA,” aliongeza.

Paula kwa upande wake alieleza furaha yake kubwa kufuatia hatua ya kuwa mama na akakiri anavyojivunia binti yake.

"AMARA❤️ 03/05/2024 Nataka tu kusema Asante Mungu🙏. Moyo wangu umejaa na shukran. Asante kwa kunichagua kuwa mama yako😍 Mungu alijua jinsi moyo wangu unakuhitaji @princess__amarah," alisema Paula.

Mamia ya wanamitandao wakiwemo mastaa wenzao tayari wamejitokeza kuwapongeza wapenzi hao kwa hatua yao mpya ya kuwa wazazi.

Tazama maoni kutoka kwa baadhi ya akaunti kwenye Instagram;

kajalafrida: Tunakupenda Mama Amara.

wemasepetu: This is beautiful. Congrats to both of you.

chino_kidd7: Ongerani sanaa jamani MUNGU amlinde kwa kila jambo na akuwe salama.

bilnass: Hongereni sana @marioo_tz @thepaulakajala #HakunaMatata

auntyezekiel: Waooh hongereni sana

Iamataleah: Mungu ni Mwema

Mwezi uliopita, wapenzi hao wawili walifichua kwamba walikuwa wakitarajia mtoto wao wa kwanza pamoja.

Wawili hao walitoa tangazo la kipekee la pamoja mapema mwezi uliopita wakifichua kwamba Paula ni mjamzito.

Walishiriki video nzuri iliyowaonyesha wakisoma gazeti lenye kichwa cha habari cha ‘A baby is on the way’ na pia kuonyesha tumbo la Paula lililochomoza.

“Ninatarajia mtoto na mpenzi wangu. Kuanzia mbili hadi tatu,” Paula aliandika chini ya video ambayo alichapisha kwenye Instagram.

Katika video hiyo, mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 22 alionekana akiwa na ujauzito mkubwa huku yeye na mpenzi wake wakionyesha picha za kijusi kinachokua tumboni mwake.

Marioo ambaye kwa jina halisi ni Omary Mwanga pia alishiriki furaha yake ya kuwa baba hivi na akamshukuru binti wa muigizaji Kajala Masaja kwa kubeba ujauzito wake.

"Kuongeza mwanachama mpya kwenye kikosi chetu! Soon inshallah.. Najivunia wewe malkia @therealpaulahkajala Mungu akubariki wewe na familia,” Marioo alisema.

Mastaa hao wawili wa bongo walianza kuchumbiana mapema mwaka jana, ikiwa ni miezi michache tu baada ya Paula kuachana na mwimbaji Rayvanny ambaye alirudiana na mzazi mwenzake, Fahymah.