Tuwache kucheza na Mungu kwa madhabahu- Lydia amwambia Kanyari

Katika taarifa yake, Wanjiru alielezea masikitiko yake na akazungumzia hitaji la kuheshimu mipaka ya kidini katika kuunda maudhui.

Muhtasari
  • Akihitimisha matamshi yake, Wanjiru alitilia shaka mawazo ya wale wanaomfuata Mchungaji Kanyari licha ya matendo yake yasiyoaminika.
Pastor Kanyari
Pastor Kanyari
Image: HISANI

Mtayarishaji wa maudhui na mjasiriamali Lydia Wanjiru amekashifu vikali video ya mtandaoni ya Mchungaji Kanyari ambayo anasema kuwa ni harakati za kutafuta kiki kwa kisingizio cha shughuli za kidini.

Maoni yake yanakuja kujibu video inayomuonyesha Mchungaji Kanyari akipokea zawadi isiyo ya kawaida kutoka kwa TikToker Faith Peters wakati wa ibada ya Jumapili.

Kifurushi hicho, kilichofungwa kwenye gazeti, kilikuwa na mjengo wa suruali ya Kotex, mafuta  ya Arimis, na pakiti ya kondomu.

Katika taarifa yake, Wanjiru alielezea masikitiko yake na akazungumzia hitaji la kuheshimu mipaka ya kidini katika kuunda maudhui.

"Katika uundaji wa maudhui tuweke madhabahu ya Mungu kando, tuwache mambo kwa kanisa, tuwache kucheza na Mungu kwa madhabahu yake," alianza, akiwahimiza waundaji wa maudhui kuweka maeneo matakatifu bila shughuli zisizo za heshima.

Wanjiru alikashifu tabia katika video hiyo, ambapo Mchungaji Kanyari anaonekana akicheka huku baadhi ya waumini wake wakipiga makofi huku wengine wakirekodi tukio hilo kwenye simu zao.

"Kumdharau Mungu kwa njia iliyo nje ya mipaka haikubaliki," alisema. “Mnafaa watu kaa hao mnachukua viboko kaa Yesu wanatoka huko nje akiwemo mchungaji.”

Alionya zaidi juu ya athari za kiroho za vitendo kama hivyo, akipendekeza kwamba vinakaribisha ghadhabu ya Mungu na bahati mbaya.

"Hivyo ndivyo watu wanavyoalika ghadhabu ya Mungu na laana, si ajabu mvua inatubeba," aliongeza, akimaanisha kuwa mafuriko ya hivi karibuni yaliyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuwa matokeo ya vitendo hivyo vya dharau.

Akihitimisha matamshi yake, Wanjiru alitilia shaka mawazo ya wale wanaomfuata Mchungaji Kanyari licha ya matendo yake yasiyoaminika.

Mbona unamfuata mtu wa namna hiyo mtu anafanya vitu kaa hizo mbele yako? How is that a person mwenye atakuja kwako akuombee ndoa yako akuombee upone?”

"Kwa nini watu wamechanganyikiwa kiasi hiki?" aliendelea, akiwapa changamoto washarika kufikiria jinsi wanavyomuunga mkono mchungaji.