"Ana kipaji na ana nidhamu, nampendelea zaidi!" Diamond ammiminia sifa kemkem Mbosso

Diamond alisema kwa maadili hayo ya kazi, Mbosso atang’aa zaidi.

Muhtasari

•"Nataka kumpongeza Mbosso, ana kipaji na ana nidhamu sana. Anafanya kazi kwa bidii na anajifunza kila wakati." Diamond alisema.

•"Anapendwa, anaimba vizuri, na hana masuala na watu. Nampendelea zaidi." alisema.

Mbosso na bosi wake Diamond Platnumz
Image: HISANI

Bosi wa WCB Diamond Platnumz amemsifia msanii wake Mbosso akimtaja kuwa ni miongoni mwa wasanii wenye nidhamu kubwa zaidi.

Akizungumza na Wasafi kwenye moja ya shoo za Mbosso, Diamond alisema staa huyo ana kipaji na anasukuma muziki wake kila wakati..

"Nataka kumpongeza Mbosso, ana kipaji na ana nidhamu sana. Anafanya kazi kwa bidii na anajifunza kila wakati." Diamond alisema.

Diamond alisema kwa maadili hayo ya kazi, Mbosso atang’aa zaidi.

"Mbosso atafika mbali sana. Maelfu ya mashabiki walikuja hapa kumtazama akitumbuiza na bado hawajampata vya kutosha."

Pia aliwashukuru mashabiki wake kwa kuwaunga mkono wasanii wa Wasafi kila mara.

“Nawashukuru sana wanaoshabikia muziki wetu, letu ni kufanya muziki halafu mashabiki wetu wasapoti vipaji vyetu.

Mbosso anaendelea kutangaza EP yake ya hivi majuzi, KHAN, iliyotolewa Oktoba mwaka huu.

Diamond alimsifu msanii huyo wake kwa kuteka hisia za watu kwa kuwaonjesha kipande cha sekunde 30 cha wimbo wa kwanza wa EP ambao sasa umesambaa kwenye mitandao ya kijamii.

"Ukiangalia wimbo wa Mbosso ambao haujatoka 'Huyu Hapa' teaser yenyewe ina zaidi ya video elfu 120 zilizotengenezwa kutoka hapo. Na wimbo huo haujatoka rasmi."

Aliongeza;

"Anapendwa, anaimba vizuri, na hana masuala na watu. Nampendelea zaidi."

Mbosso alitambulishwa rasmi kama mtia saini wa Wasafi Classic Baby (WCB) Februari 2018.

Hapo awali, Mbosso alikuwa chini ya bendi ya Yamoto.

Mbosso alijiunga na WCB baada ya kundi lake la zamani kusambaratika huku kukiwa na tetesi za kutoelewana na uongozi wao.

Yamoto ilikuwa inasimamiwa na Mkubwa Fella.

Katika mahojiano yaliyopita, Rayvanny alisema yeye ndiye aliyemshawishi Diamond kusaini Mbosso kwa Wasafi.

“Mbosso Lava Lava ni watu ambao walinikuta Wasafi na pia nilikuwa nawaambia kukata tamaa kila kitu kinaenda sawa. Na nilikuwa naongea na Diamond bhana Mbosso yupo vizuri lakini hana Management tumsaidiae, mimi ndio nimelazimisha hadi Mbosso amefika pale,” said Rayvvnny.

(Utafsiri: Samuel Maina)