Msimshambulie dada yangu wala Nelly Oaks!- Akothee awasihi wanamitandao

Akothee alizungumzia vurugu iliyomo baina yake na dada yake

Muhtasari

• Alisema kuwa yeye hana ubaya na dada yake ila akawaagiza mashabiki wake wasimburute   kwenye ukurasa wake.

•Aliwaomba watu wanaozozana katika familia zao kutatua tofautizao  kwani familia hazifai kuvunjika.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki Akothee amesema kuwa ugomvi ulioko baina yake na familia yake ni ugomvi wa kindugu.

Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, alisema amekuwa akizozana na dada yake Cebbie kwa muda wa takriban mwaka mmoja sasa baada ya kutokea ugomvi wa kifamilia.

Aliongeza kuwa yeye hana ubaya na dada yake ila akawaagiza mashabiki wake wasimburute   kwenye ukurasa wake.

"Nilikusanya virago vyangu na nikaondokea uhusiano wangu na dada yangu mwezi wa Desemba. Kuna harusi itakayokuwa mwaka huu Desemba na nimekuwa nikifurahia hatua hiyo, nawatakia mema, hata hivyo sikuwa niende kwenye harusi hiyo," Akothee alisema akiwa amejawa na  ghadhabu.

Aliwaomba mashabiki wake waendelee kumuunga mkono Cebbie anapofanya vizuri ila wasimshabikie kwenye ukurasa wake.

Akothee alisema kuwa kuna muda ambao hakuwa sawa kiafya na alikuwa akijikaza ili aweze kuwa sawa. Amewaomba watu wakiwemo wanafamilia kumwacha  na kuwaomba wasiingilie ugomvi uliopo kati yake na dadake.

"Sijasema kuwa yeye ni mtu mwenye maovu. Nilikuwa na msongo wa mawazo kwa miezi 6 nikipigania hali hiyo ya huzuni. Nilivunja mahusiano mengi na kukusanya virago vyangu ili kuweza kuwa sawa," mwanamuziki huyo alisema.

Aliongeza kuwa yeye na dadake wamepata wachumba kwa wakati mmoja na kuwa hana shida na hilo wala kutaka kushindana naye. Alisema kuwa alitarajia kuwa mama yake angeelewa na kuwa angewakubali na kufurahia uchumba wao wawili.

Mwanamuziki huyo aliwaomba watu wanaozozana katika familia zao kutatua tofautizao  kwani familia hazifai kuvunjika.

"Ningekuwa katika nafasi ya mama yangu ya kuwa na mabinti wawili ambao wanatarajia kupiga hatua kubwa kwenye mahusiano yao, ningekuwa na furaha sana," Akothee alieleza hali yake na familia yake.

Aliongeza kuwa sababu ya kuzozana na dada yake ni  kuwa mdogo wake alilalamika kwamba huwa hamtetei anapovamiwa na maoni ya wanamitandao.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa yeye hajui jinsi ya kumtetea dadake mtandaoni dada yake wakati amesambaza fununu kumhusu,

"Sasa nawaomba msimvamie dada yangu kwenye mtandao. Alikuwa anadanganya na alikubali kuwa madai hayo hayakuwa ya kweli," Akothee alisema.

Aliongeza pia kuwa watu wasiwavamie dada yake na mpenzi wake wa hapo awali Nelly Oaks na kuwa hataki kutetewa kivyovyote vile na familia yake.