Mulamwah aonywa vikali kwa kumshika Diana Marua kimapenzi

"Wewe ni mzuri. Unakaa fiti. Suti umeweka, umeiva, unakaa poa," Diana alimsifia Mulamwah.

Muhtasari

•Mulamwah pia alisifia urembo wa mama huyo wa watoto watatu kabla ya Dr Ofweneke kukatiza mkutano wao mzuri.

•Mchekeshaji Eddie Butita hakusita kumkumbusha Mulamwah kwamba rapa huyo ni mke wa Bahati.

Diana Marua akutana na Mulamwah
Image: HISANI

Mwanavlogu Diana Marua na mchekeshaji David Oyando almaarufu Mulamwah walikutana kwa mara ya kwanza siku ya Jumanne.

Wawili hao walikutana wakati wa kurekodi kipindi cha Mr Right kwenye Rembo TV ambacho Diana anaanda pamoja na Dr Ofweneke. 

Mulamwah alichapisha video fupi ya mkutano wao wa kwanza ambapo walionekana kufurahi sana kuweza kuonana hatimaye.

"Hatimaye nimekutana na Mulamwah. Sijawahi kumuona uso kwa uso. Huwa namuona tu kwa mitandao," Diana alisema.

Katika video hiyo, Mulamwah alionekana  akimshika mke huyo wa mwimbaji Bahati kwenye kiuno. Diana Marua pia alimshika mchekeshaji huyo shingoni huku wawili hao wakisherehekea mkutano wao kwa furaha.

Rapa huyo alimshukuru Mulamwah kwa kukubali wito wao kwenye kipindi hicho kabla ya kusifia mwonekano na mavazi yake.

"Wewe ni mzuri. Unakaa fiti. Suti umeweka, umeiva, unakaa poa,"  Diana alisikika akimwambia baba huyo wa binti mmoja.

Mulamwah pia alisifia urembo wa mama huyo wa watoto watatu kabla ya Dr Ofweneke kukatiza mkutano wao mzuri.

Makumi ya wanamitandao walikuwa wepesi kutoa maoni yao chini ya video hiyo huku sehemu yao ikimuonya mchekeshaji huyo kwa jinsi alivyomshikilia Diana. Mchekeshaji Eddie Butita hakusita kumkumbusha kwamba rapa huyo ni mke wa mtu.

"Wewe wacha kushika bibi ya Bahati hivyo!" Butita alionya.

Mulamwah alijibu, "Usimtag."

Anayedaiwa kuwa mpenzi wa sasa wa Mulamwah, Ruth K alisema, "Hii imeenda."

Baadhi ya watumizi wa Instagram walimualika Bahati kwenye ukurasa wa mchekeshaji huyo kushuhudia yaliyo kwenye video.

iannoh: Bahati typing.. and deleting..

offici_alpierre Nangoja comment ya Bahati

its_firewest Umeshika kiuno na hutaki kumuachilia. Bahati njoo uone hii.