Harmonize na dadake Diamond waonyeshana upendo mkubwa waziwazi, Kunani?

"Je, watu wanaonekana bora wakati wapo single? @_esmaplatnumz," Harmonize alihoji.

Muhtasari

•Harmonize amependa kitendo cha dada mkubwa wa Diamond, Esma Platnumz  kurekodi video akifurahia wimbo wake  ‘Single again.’

•Esma alionekana kupendezwa na maneno ya wimbo huo ambao unazungumzia maisha ya mtu asiye na mchumba.

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Harmonize amependa kitendo cha dada mkubwa wa Diamond, Esma Platnumz  kurekodi video akifurahia wimbo wake mpya ‘Single again.’

Katika video fupi ambayo bosi huyo wa Kondegang alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Esma anaonekana akifurahia wimbo huo uliotolewa siku ya wapendanao na hata kuimba baadhi ya maneno yake.

Dada huyo wa bosi wa zamani wa Harmonize na ambaye ni hasidi wake mkubwa zaidi wa sasa alionekana kupendezwa na maneno ya wimbo huo ambao unazungumzia maisha ya mtu asiye na mchumba.

"Je, watu wanaonekana bora wakati wapo single? @_esmaplatnumz," Konde Boy alihoji na kuambatanisha na emoji ya upendo.

Katika video nyingine ambayo inavuma kwenye mitandao ya kijamii, Esma anaonekana pamoja na mwanamke mwingine ndani ya gari akiimba sehemu ya wimbo huo ambao uliotolewa siku ya Jumanne.

“Masingle lady mmeona? Mimi kila siku niko single, sijui mwenzangu. Hadi siku ya Valentine's tupo single" alisikika akisema huku wimbo huo ukiendelea kucheza kwenye redio ya gari.

Mama huyo wa watoto watatu alionekana kuufurahia sana wimbo huo na hata alisikika akiimba pia huku wimbo ukiendelea kucheza.

Katika sehemu ya wimbo huo ambao umekuwa ukivuma kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki, Harmonize anaimba, "I'm single. Do you know that I'm single? I'm single again! Who knows that I'm single? Ooh yes, I'm single. Ladies I'm single again!I 'm single. Who knows I'm single?"  ("Mimi niko single. Je, unajua niko single? Niko single tena! Nani anajua kuwa mimi niko single? Ooh kweli, niko single. Wanawake niko single tena. Niko single. Nani unajua mimi niko single?")

Esma amekuwa kwenye mahusiano kadhaa na hata ameolewa mara mbili Takriban miaka mitatu iliyopita, aligura ndoa yake na mfanyibiashara Yahya Msizwa miezi michache tu baada ya kufunga pingu za maisha.

Siku za hivi majuzi, Harmonize amekuwa akiweka wazi kwamba hayupo kwenye mahusiano yoyote baada ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake, muigizaji Frida Kajala Masanja mwishoni mwa mwaka uliopita.

Mapema mwezi huu, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alisema kwa sasa anajipatia muda usiojulikana wa mapumziko kabla ya kujitosa kwenye mahusiano mapya.

"Msijali, hivi karibuni nitapata mtu na mtamjua!!," alisema.

Staa huyo wa Bongopia alidokeza kwamba alipitia masaibu mengi mno wakati akiwa katika mahusiano yake ya awali.