Wanawake wenye furaha zaidi ni wale ambao walifanya uchaguzi wa kujipenda wenyewe-Esther Musila

Muhtasari
  • Mkewe msanii  wa Injili wa Kenya Guardian Angel, Esther Musila sasa ametoa ushauri kwa wanawake, walioolewa au ambao hawajaolewa, siku chache baada ya harusi yake na Guardian Angel
Image: INSTAGRAM// GUARDIAN ANGEL

Mkewe msanii  wa Injili wa Kenya Guardian Angel, Esther Musila sasa ametoa ushauri kwa wanawake, walioolewa au ambao hawajaolewa, siku chache baada ya harusi yake na Guardian Angel.

Musila alichapisha video ya siku yake ya harusi kwenye Instagram siku ya Jumapili, pamoja na ujumbe mrefu wa kishairi ulioelekezwa kwa wanawake.

Mama huyo wa watoto watatu aliendelea kufafanua mwanamke mwenye furaha ni nani, ambapo aliandika, wanawake wenye furaha zaidi hawajaolewa na pia sio waseja.

Musila aliendelea kusema kuwa wanawake wenye furaha hawachezi wahasiriwa bali hupitisha hasira zao na kuchagua furaha.

"Wanawake wenye furaha zaidi leo sio wale walioolewa. Sio wale wako 'single'. Sio wale walio na kazi thabiti na mapato mazuri

Wanawake wenye furaha zaidi ni wale ambao walifanya uchaguzi wa kujipenda wenyewe kabisa na kweli. Wanawake ambao walichagua kuacha ya zamani walijitahidi kujistahi na kuweka bei ya juu juu ya kujistahi kwao.

Waliacha kucheza wahasiriwa. Waliacha kunung'unika kwa kujihurumia na kula katika karamu za huruma.

Walipitia hasira, machozi na uchungu wao. Walitambua kwamba furaha ni chaguo na wajibu wa kibinafsi. Walichagua kufafanuliwa na maisha yao ya sasa, lakini sio maisha yao ya zamani,"Aliandika Musila.

Musila aliongeza kuwa wanawake wenye furaha hawahitaji kumtupia mtu yeyote kivuli ili kung’aa.

"Wana furaha kwa sababu hawahitaji uthibitisho kutoka kwa mtu yeyote. Wana furaha kwa sababu wanajua kwamba hawana haja ya kutupa kivuli kwa mtu yeyote ili wao kuangaza. Wana furaha kwa sababu walichagua kuwa Queens, kwa wanawake wa nyumbani…”