Mambo ni mazito! Nuh Mziwanda aomba kurudiana na Shilole

Muhtasari

• Msanii Nuh Mziwanda amaedokeza kwamba angetaka kurudiana na mpenzi wake wa zamani, Shilole.

• Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, inaonekana mwanamuziki huyo anampeza Shilole na angependa kivyovyote vile warudiane ili waendeleze penzi lao kama zamani.

Nuh Mziwanda
Nuh Mziwanda
Image: Instagram KWA HISANI

Msanii Nuh Mziwanda amaedokeza kwamba angetaka kurudiana na mpenzi wake wa zamani, Shilole.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, inaonekana mwanamuziki huyo anampeza Shilole na angependa kivyovyote vile warudiane ili waendeleze penzi lao kama zamani.

Amewauliza mashabiki wake iwapo wangependa kuwaona pamoja huku wakitoa maoni tofauti kuhusu ishu hiyo. Hili linajiri siku chache baada ya msanii huyo kuposti kwenye mitandao yake ya kijamii akidai kwamba aliwatengenezea mazingira mazuri wapenzi wote wa Shilole waliokuja baada yake na kusema kwamba yupo tayari kusonga mbele na maisha yake.

Ifahamike kwamba Shilole yupo katika mahusiano kwa sasa na mpenzi wake, Rommy ambaye ni mpigapicha maarufu huko Tanzania.

Mashabiki wanasubiri kuona iwapo Shilole atazungumza jambo lolote kuhusu kauli hiyo ya Mziwanda na iwapo mumewe anahisi vipi kuhusu visanga hivi vya kila siku vinavyomuandama mkewe.