Lillian Ng'ang'a azindua kumbukumbu ya maisha yake kama mke wa gavana

Muhtasari

• Aliyekuwa mke wa gavana wa Machakos, Lillian Ng’ang’a ametangaza kuachia kumbukumbu kuhusu Maisha yake alivyokuwa mke wa gavana wa Machakos Alfred Mutua.

•Ni kumbukumbu ambayo inazungumzia ukweli kuhusu maisha yake vile alivyojipata kwenye umaarufu wa mitandaoni, alichokifanya kama mke wa gavana na matukio ya baada na kabla ya kutengana

Lillian Ng'ang'a
Image: Instagram

Aliyekuwa mke wa gavana wa Machakos, Lillian Ng’ang’a ametangaza kuachia kumbukumbu kuhusu Maisha yake kwa jumla kama mke wa gavana wa Machakos Alfred Mutua.

Ng’ang’a ambaye walitengana na Mutua mwaka jana ametangaza kwamba ataiachia kumbukumbu hiyo ambayo ameibatiza kwa jina ‘Madam First Lady’ ambapo amezungumzia Maisha yake alivyojipata katika umaarufu wa mitandaoni, huku kukiwa na mazungumzo mengi kuhusu uhusiano wake na gavana, kuafikia mambo mengi kama mke wa gavana, na hadi kuachana kulikoambatanishwa na matukio mengi.

“Hii ni kumbukumbu ambayo ninaienzi sana katika kitabu kinachosheheni hadithi yangu ambapo ninachukua usukani kama msimulizi na kusimulia ukweli wangu,” aliandika Ng’ang’a kwenye Instagram yake.

Image: INSTAGRAM

Alielezea kwamba tarehe ya kuachia kumbukumbu hiyo ilipangwa na mpenzi wake wa pili ambaye siku zote anamtaja kama ‘my significant no #2’ ambaye kila mtu anajua vizuri ni mwanamuziki wa kufoka Juliani.

Ng’ang’a amewataka wafuasi na mashabiki wake kujichukulia kumbukumbu hiyo kwa wingi ili kupata kujua ukweli wa Maisha yake alipokuwa akihudumu kama mke wa gavana wa Machakos na pia amewataka wachukulie hata marafiki ili kuieneza Zaidi.

Wiki chache zilizopita palizuka uvumi kwamba Ng’ang’a na Juliani walifunga harusi katika hafla iliyoandaliwa faraghani na baadae kuende Mombasa kwa fungate ambapo waliachia picha na watu wengi kusema kwamba Ng’ang’a ni mjamzito kwa kile walichokiona katika picha hizo.