"Nianze na gani?" Nandy kutoa kibao cha kwanza baada ya kimya kirefu

Muhtasari

• Baada ya kimya cha mwezi mmoja bila kuachia muziki wowote, hatimaye msanii kutoka taifa jirani la Tanzania , Nandy amedokeza kwamba atakuwa anaachia ngoma ambazo amekuwa akiziandaa.

• Nandy kwa upande wake amewahakikishia mashabiki wake kwamba, wimbo wa kwanza atakaoachia ni ule ambao utachaguliwa na asilimia kubwa ya mashabiki.

Baada ya kimya cha mwezi mmoja bila kuachia muziki wowote, hatimaye msanii kutoka taifa jirani la Tanzania , Nandy amedokeza kwamba atakuwa anaachia ngoma ambazo amekuwa akiziandaa.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Nandy aliwauliza mashabiki wake kuhusu kibao ambacho wangependa aachie cha kwanza huku akitoa orodha ya ngoma ambazo amesharekodi.

“Hivi kulingana na hisia zako, unahitaji kusikia wimbo gani kutoka kwangu?” Nandy aliuliza.

Baadhi ya vibao ambavyo huenda tukashuhudia kutoka kwa kichuna Nandy ni pamoja na:

  • Ya maumivu
  • Mapenzi [Kupendana]
  • Kucheza [Club]

 

Nandy kwa upande wake amewahakikishia mashabiki wake kwamba, wimbo wa kwanza atakaoachia ni ule ambao utachaguliwa na asilimia kubwa ya mashabiki.

Hatua hii ya Nandy inajiri siku chache tu baada ya kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, Billnass huku ikitarajiwa kwamba watakuwa wanafunga ndo hivi karibuni.

‘The African Princess’, ni miongoni wa wasanii wa kike ndani ya Tanzania na Afrika Mashariki ambao wamejituma na kupiga hatua kubwa katika gemu la burudani.