'Labda Diamond na Harmonize wanaongea, hawana ugomvi' - S2Kizzy

Muhtasari

• Msalishaji wa muziki, S2Kizzy alisema kwamba Diamond na Harmonize ni marafiki kutoka kitambo na kwamba kile kinachoenezwa mitandaoni kuwa ni ugomvi baina yao ni hasira tu na zikiisha huenda watafanya kazi pamoja.

S2kizzy
Image: Instagram

Msalishaji wa muziki nchini Tanzania, S2Kizzy ameibua madai kwamba huenda beef kati ya msanii Diamond Platnumz na Harmonize ni kiki tu za mitandaoni na kusema kwamba wawili hao huenda nyuma ya pazia ni marafiki na wanaongea.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na mwanablogu mmoja nchini humo, S2Kizzy alisema kwamba wasanii hao huenda wanaongea na hawana ugomvi jinsi ambavyo mashabiki na wafuasi wao wengi wanavyochukulia.

Yeye alijitenga na kuegemea upande wa yeyote kwa kusema kwamba hatua yake hiyo ni kutokana na kwamba hapendi ugomvi na nia yake ni kuona wasanii wote wakiwa wamependana na kufanya kazi Pamoja ili kusukuma muziki wa Afrika Mashariki mbele Zaidi.

“Mimi sipendi maugomvi ndio maana sina timu. Napenda wasanii wapendane na wasapotiane, muziki wetu uende mbali Zaidi,” alisema S2Kizzy.

Msalishaji huyo mahiri wa miziki ya kizazi kipya alisema kwamba hana habari kabisa kama Diamond na Harmonize wana ugomvi na kudokeza kwamba pengine huwa wanaongea.

“Mimi sijui kama wana ugomvi, labda wanaongea. Huwezi kujua, labda wanaongea, na suala la ugomvi sasa ni watu wanaona vile, lakini wanaweza kuwa wanaongea pia. Hao ni wat utu wanaona kama wanagombana lakini mimi naona love tu kwa sababu Diamond amemtoa Harmonize kimuziki kwa sababu alikuwa anampenda, wanapendana. Upendo ukizidi sana baadae inakuwa kwamba watu hadi wanakwaruzana, kwa hiyo ni misunderstanding tu,” alisema S2Kizzy.

Alipoulizwa kama labda amewahi tengeneza beat na akawaza wawili hao kuungana na kufanya muziki na beat hiyo, S2Kizzy alisema kwamba beat ziko nyingi tu na akadokeza kwamba huu mwaka wa 2022 kuna shughuli kibao matamasha na hafla mbalimbali lakini akasema kwamba hajui kama Diamond na Harmonize watakutana Pamoja kwa collabo. Ila alisisitizazaidi kwamba wawili hao wanapendana Zaidi ya maelezo.

“Wale watu wametoka mbali, wametoka mbali sana wale na sisi hatuwajui kama wao wanavyojuana, wametoana mbali miaka kibao. Hii miaka miwili sioni kama ni hamna, mbona watu hawaongei miaka mitatu minne. Inakuwa tu kama wamechukia, hasira zikiisha, freshi. Ni mtu na mtoto wake, kawaida,” alisema S2Kizzy.