Milly wa Jesus asutwa kwa kuiga muonekano kama wa Rihanna

Muhtasari

• Familia ya Wa Jesus imegeuzwa gumzo la mitandaoni baada ya kupakia picha ya Milly akiwa amevaa kama Mwanamuziki Rihanna.

Rihanna, Milly Wa Jesus
Image: Instagram

Mwanablogu wa mtandao wa YouTube nchini Kenya MillywaJesus amesutwa na wanamitandao baada ya kuvalia kama mwanamuziki mashuhuri duniani Rihanna.

Milly Pamoja na mumewe Kabi walipakia picha na video zake hizo akiwa amwevalia kama Rihanna huku ameachia tumbo wqazi ili kuonesha ujauzito wake, kama ambavyo alifanya Rihanna mwezi uliopita akiweka wazi kuhusu ujauzito wake na msanii A$ap Rocky.

Kwa upande wake Kabi aliipakia video hiyo akiwauliza wafuasi na mashabiki wake kwamba wanasema anafanana na Rihanna. Watu walishuka katika post hiyo ya kumkashfu kwa kujifananisha msanii mkubwa kama Rihanna.

Ati watu wanasema @millywajesus anafanana na Rihanna? Sijui nani alimwambia hivyo but she actually believes it hadi akaenda @fiestahousematernity kufanywa Photoshoot ya look alike,” aliandika Kabi wa Jesus.

Kwenye video hiyo, Milly anasikika akisema si yeye amejifananisha na Rihanna bali ni watu wamesema hivo

“Anaonekana vizuri lakini hapo kwa Rihanna zii,” mmoja aliandika huku mwingine akimchamba kwamba mimba ya Rihanna imeenda shule.

Kwa upande wake Milly wa Jesus alipakia kwenye Instagram yake na kusema kwamba watu wanamuita Mirihanna.

“Ati mnaniita aje “good girl Milly” “Mirihana” “Good girl Riri” na gani ingine?” aliandika Milly.

Wazo lako ni lipi kuhusiana na muonekano wa Milly na Rihanna?