Melinda Gates azungumzia talaka ya ndoa na Bill Gates

Muhtasari

• Baada ya kimya cha muda mrefu, Belinda Gates hatimaye amefunguka kuhusu kiini cha kuvunjika kwa ndoa yake ya miaka 27 na mumewe tajiri Bill Gates.

• Melinda anasema urafiki wa Bill Gates na mwanaume Jeffrey Epstein ambaye kwake alikuwa na muonekano wa kutisha ndicho chanzo cha kukosa maelewano baina yao.

Bill Gates, Melinda Gates
Image: BBC News//getty Images

Aliyekuwa mke wa tajiri namba tatu duniani Bill gates, Melinda Gates kwa mara ya kwanza amefunguka kiini cha kuvunjika kwa ndoa yake ya miaka 27 na mkwasi huyo katika mahojiano ya kipekee na runinga moja nchini Marekani.

Melinda anasema kwamba hakuwa anaamini kile walichokuwa wakimiliki na Bill Gates na kumtuhumu mume wake wa zamani kwa kile alisema ni kusisitiza kukutana na mwanamume kwa jina Jeffrey Epstein ambaye Melinda awali alikuwa amemuota vibaya kutokana na muonekano wake wa kutisha.

Aidha katika mahojiano hayo, Melinda alisema kwamba yeye alijaribu sana kuona ndoa yao inasimama na kudumu milele lakini ilishindikana na kusema kwamba yeye hajutii kwa sababu alijitolea kwa hali na mali lakini ni kama halikuandikwa na hivyo halingetimia.

Melinnda alifunguka kwamba ugomvi wao ulianza mwaka wa 2011 wakati Bill alitaka kuonana na mwanaume huyo kwa jina Jeffrey na alipomkataza kwa kumuota vibaya, Bill alisisitiza kuonana na yeye na hapo Melinda akawa na mashaka Zaidi.

“Sikupenda kwamba alikuwa na mikutano na Jeffrey Epstein. Nilimweleza jambo hilo wazi. Pia nilikutana na Jeffrey Epstein wakati mmoja haswa. Nilitaka kuona mtu huyu alikuwa nani na nilijuta kutoka kwa sekunde niliyoingia mlangoni. Alikuwa mtu wa kuchukiza, mwovu. Niliota ndoto mbaya baadaye. Ndiyo maana moyo wangu unavunjika kwa ajili ya wasichana hawa. Hivyo ndivyo nilivyohisi, na mimi ni mwanamke mzee. Alikuwa mbaya sana,” alisema Melinda.

 

Melinda Gate alisema kwamba mikutano ya mumewe wa zamani na Epstein ambaye kwake yeye alimuona kama mtu mwenye muonekano wa kijabau kama janabi ilichangia sana kuzua mkwamo mkubwa wa kimahusiano na Bill Gates.

Alimwambia mtangazaji Gayle King kwamba kila mara Bill walipokutana na Epstein, alilazimika kujibu maswali mengi mbele yake na ambapo alikuwa akishindwa na kuchangia ndoa yao kukosa mwafaka kabisa Zaidi ya talaka.