Sikutegemea tuachane na Mulamwah, nilitaka 'future' naye - Carrol Sonie

Muhtasari

• Carrol Sonie amesema kwamba alikubali kumbebea mtoto Mulamwah kwa sababu alikuwa anataka 'future' na mchekeshaji huyo lakini mambo yakatokea kivingine.

Carrol Sonie
Image: Facebook

Muigizaji Carrol Sonie hatimaye amefunguka kuhusu uhusiano wake uliovurugika na mchekeshaji Mulamwah.

Katika mahojiano ya kipekee na Dr. Ofweneke, Sonie alisema kwamba alikuwa anampenda Mulamwqah kw asana na ndio sababu kubwa yake yeye kukubali kulea mimba yake, kinyume na ambavyo imekuwa ikisambazwa mitandaoni kwamba mimba hiyo haikuwa ya Mulamwah.

Akiulizwa ni nini kilimfanya akampenda Mulamwah, Sonie alimsifia mchekeshaji huyo na kumtaja kuwa mtu muungwana na mwenye alimpa shavu na kumsaidia kukua kisanaa kama muigizaji.

“Mimi sikuwa nategemea tuachane na pia kukubali kumbebea mtoto, it means a lot. Nilikuwa nataka mustakabali na yeye na pia nilikuwa nataka sana tukue Pamoja kwa sababu mahusiano yetu yalidumu kwa takriban miaka minne na hivyo alikuwa anajua mapungufu yangu na ueledi wqangu, nami pia vile vile. Mimi kusema kweli nilitaka sana tuwe Pamoja lakini mambo yakitokea,” alisema Sonie.

Muigizaji huyo aidha amesisitiza kwamba kwa sasa ameshajipa shughuli na maisha na amemsahau Mulamwah katika maisha yake kwa sabqabu hayo kwake ni kama matukio ya kitambo.