Mwijaku amtaka Alikiba kumuoa Shilole kama mke wa pili

Muhtasari

• Mtangazaji na mfanyibiashara kutoka Tanzania, Mwijaku amemtaka Alikiba kumuoa Shilole kama mke wa pili.

• “Alikiba na Shilole breki hazikabi, namshauri amuoe mke wa pili,” Mwijaku alisema.

Mtangazaji Mwijaku
Mtangazaji Mwijaku
Image: hisani

Mtangazaji na mfanyibiashara kutoka Tanzania, Mwijaku amemtaka Alikiba kumuoa Shilole kama mke wa pili.

Akizungumza katika mahijiano na CarryMastory, Mwijaku alisema kwamba wawili hao ni rafiki wa karibu na wanaweza kuwa wapenzi wa kupigiwa mfano.

“Alikiba na Shilole breki hazikabi, namshauri amuoe mke wa pili,” Mwijaku alisema.

Kauli hii ya ‘DC wa Instagram’ inajiri baada ya video kusambaa mitandaoni ikionyesha Shilole akiwa amemkumbatia Alikiba wakiwa kwenye jukwaa.

Ifahamike kwamba ni siku chache tu zilizopita ambapo mkewe Alikiba, Amina Khalef kuomba talaka akisema kwamba hataki tena kusukuma gurudumu la ndoa na msanii huyo mkubwa Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Shilole, tayari ana mpenzi wake, Rommy ambaye wameonekana kunogesha penzi lao hasahasa kupitia picha ambazo mara kwa mara wamezipakia katika mtandao wa Instagram.

Kwa sasa mashabiki na washikadau wa burudani watalazimika kusubiri kuona iwapo kauli hiyo ya Mwijaku itasambaratisha ndoa ya Shilole.