Hao ni maskini acha waongee, Cassavera ni yangu - KRG

Muhtasari

• Msanii na mfanyibiashara KRG the Don amefutilia mbali madai ya  mashabiki wanaosema sehemu  ya starehe ya Cassavera sio yake na kwamba ameajiriwa tu kama balozi.

• “…Ni sawa, anayezungumza ni nani? Hakuna siku nimeingia hapa nikafukuzwa, kwa hiyo sijui wanasema nini,” alisema.

 

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: KRG the Don

Msanii na mfanyibiashara KRG the Don amefutilia mbali madai ya  mashabiki wanaosema sehemu  ya starehe ya Cassavera sio yake na kwamba ameajiriwa tu kama balozi.

 Akizungumza katika mahojiano kwenye Obinna tv, KRG alisema kwamba wengi wa wale wanaozungumza ni masikini ambao wameshindwa kuboresha maisha yao na kuleta machungu yao kwake.

“…Ni sawa, anayezungumza ni nani? Hakuna siku nimeingia hapa nikafukuzwa, kwa hiyo sijui wanasema nini,” alisema.

KRG alisisitiza kwamba atazidi kufanya biashara zake na kupata hela huku watu wakiendelea kuzungumza mambo yasiyo kweli.

Alisema kwamba kinachomsaidia kutasua katika maisha ni uwezo wake wa kujenga uhusiano mzuri na watu waliofanikiwa katika maisha ambao baadaye wanampa ujanja wa kutengeneza mali nyingi.

Mwanamuziki huyo alisema kwamba alianza kupata mali yake kitambo, kwani mwaka wa 2014 tayari alikuwa na shilingi milioni 200 kwenye benki.