Butita asema wasanii 'wanasota' kwa kutumia dawa za kulevya

Muhtasari

• Eddie Butita amesema wasanii wengi wanatumia dawa za kulevya.

• Aidha alisema kwamba ni asilimia ndogo sana ya wasanii ambao wanapata pesa nyingi kutoka kwa muziki, na pindi wanapozipata wanazitumia vibaya.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Eddie Butita

Mcheshi Eddie Butita amesema kwamba wasanii na watu wengi maarufu wanajikuta matatani na kuishi maisha ya dhiki kwa kutumia vileo na dawa za kulevya.

Akizungumza katika mahojiano na mwanablogu Mungai Eve, Butita alisema kwamba wengi wa wasanii wanasumbuliwa na shinikizo la kutaka kufurahisha mashabiki na kuonyesha ubabe wao bila kufahamu kwamba wanajiharibia maisha.

"...Jambo la kwanza, wasanii wengi wanaumia lazima utapata wanatumia vileo," Butita alisema.

Aidha alisema kwamba ni asilimia ndogo sana ya wasanii ambao wanapata pesa nyingi kutoka kwa muziki, na pindi wanapozipata wanazitumia vibaya.

Butita alisema kwamba ku na wale wasanii ambao pia waligeuka maskini ghafla kwa sababu ya matatizo [kama ugonjwa, kusaidia familia] , akisema hilo linaeleweka.

Aliwataka wasanii wote kuwa na watu ambao watawasaidia kupanga mikakati ya maisha na muziki wao ili wasije kuhangaika baada ya kipindi chao cha umaarufu.