Bahati kuwania ubunge wa Mathare kwa tikiti ya Jubilee

Muhtasari

• Msanii Bahati ametangaza kuwania ubunge wa eneo la Mathare kwa tikiti ya Jubilee.

• Hili linajiri wakati wasanii kadhaa wamejitokeza kuingia katika siasa za mwezi Agosti.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Bahati

Hatimaye msanii Kevin Bahati ametangaza rasmi kwamba atawania ubunge wa eneo la Mathare kupitia tikiti ya chama cha Jubilee katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Bahati alikaribishwa katika chama hicho na mkrugenzi wa uchaguzi, Kanini Kega.

Msanii huyo alisema kwamba amefanya uamuzi huo baada ya kupokea wito kutoka kwa wakazi wa eneo hilo ambao walimtaka kuwawakilisha bungeni.

Aidha alisema kwamba kwamba kwa miongo mitatu iliyopita, eneobunge la Mathare halijakuwa na kiongozi ambaye amezaliwa na kulelewa katika eneo huku akijitwika jukumu la kuwawakilisha wananchi hao.

Msanii  huyo aliahidi kwamba atawahudumia wakazi wote kwa usawa na kuleta maendeleo katika eneo hilo.

Amesema kwamba alifanya mashauriano na washikadau wengi katika eneo hilo kabla ya kuchukua hatua hiyo ambayo inatarajiwa kuibua hisia changamano katika mitandao ya kijamii.