Daktari alikuwa ametuonya tujiepushe na ngono nilipopata ujauzito- Nadia Mukami

Muhtasari

•Nadia Mukami amefichua kwamba mwanawe alitungwa tumboni mwake katika kisiwa cha Zanzibar.

•Wazazi hao wa mtoto mmoja walifichua ingawa walikuwa wamekasirikiana kabla ya safari ziara yao ya Zanzibar, waliponda raha kweli walipokuwa katika kisiwa hicho.

Image: INSTAGRAM// NADIA MUKAMI

Malkia wa muziki wa kisasa Nadia Mukami amefichua kwamba mwanawe alitungwa tumboni mwake katika kisiwa cha Zanzibar.

Wakizungumza kupitia mtandao wa Youtube, Nadia na Arrow Bwoy walisema wakati huo walikuwa wameenda kurekodi video ya kibao chao 'Raha'

Katika kipindi ambapo wawili hao walifunga safari ya kuelekea Zanzibar hali ya wasiwasi ilikuwa imeingia mahusiano yao kwani hata hawakuwa wanazungumza.

"Nilikuwa nimepitia mwaka mbaya. Kuna mengi yaliyokuwa yanaendelea. Daktari alikuwa ametuambia tujiepushe na ngono. Alitwambia si lazima. Lakini kipindi daktari alituambia tujiepushe na mapenzi ndipo tulienda kurekodi video ya 'Raha' huko Zanzibar. Mengine ni historia," Nadia alisimulia.

Wazazi hao wa mtoto mmoja walifichua ingawa walikuwa wamekasirikiana kabla ya safari ziara yao ya Zanzibar, waliponda raha kweli walipokuwa katika kisiwa hicho cha Bahari la Hindi.

"Tulikuwa na raha kupitiliza. Tungeita mtoto wetu Zanzibar. Nilimwambia (Arrow Bwoy), nisipopata ujauzito hapa basi hana uwezo wa kuzalisha," Nadia alisema.

Nadia hata hivyo alisema hana uhakika kuhusu tarehe rasmi ambapo ujauzito wake ulitungwa tumboni.

Alisema aligundua ujauzito wake mnamo Agosti 28, 2021. Wakati huo tayari alikuwa ameubeba kwa takriban wiki sita.