Diamond azungumza baada ya akaunti yake ya Youtube kurejeshwa

Muhtasari
  • Chaneli ya Diamond Platnumz, ambayo ina watumiaji zaidi ya milioni 6.5 na yenye kutazamwa na watu zaidi ya bilioni moja, ilisemekana kuwa ilidukuliwa siku ya Jumapili
Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Staa wa bongo Diamond Platnumz siku ya Jumatatu alipata pigo kubwa baada ya chaneli yake ya Youtube kudukuliwa.

Chaneli ya Diamond Platnumz, ambayo ina watumiaji zaidi ya milioni 6.5 na yenye kutazamwa na watu zaidi ya bilioni moja, ilisemekana kuwa ilidukuliwa siku ya Jumapili.

Afisa wa kampuni ya rekodi ya Diamond Platnumz, Wasafi, alisema kuwa walipokea barua pepe kutoka YouTube ikiwajulisha kuwa akaunti hiyo imesimamishwa.

Majid Ramadhani alisema ilisitishwa baada ya wadukuzi hao kuweka wazi maudhui ambayo yalikiuka miongozo ya jukwaa la kidigitali.

Siku ya Jumatatu, nyota huyo wa muziki aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akionyesha kuwa ukurasa huo umerejea.

"Asante wapenzi wangu....chaneli yangu ya Youtube imerejea," alisema.

Chaneli hiyo ina wafuasi zaidi ya milioni 6 na kumfanya Diamond kuwa kati ya wasanii wenye wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao wa Youtube barani Afrika.