YY amrukia shabiki aliyemwambia ana runinga ndogo hali ya kuwa yeye ni Mjaluo

YY hakusita kumpa jibu mwafaka lililomzima kabisha shabiki huyo mwenye nongwa mitandaoni.

Muhtasari

• Shabiki huyo alisema kwamba YY anamiliki runinga ndogo kinyume cha kawaida ya wajaluo kumiliki vitu vikubwa

• “Hivi unajua ni kwa nini wewe una runinga kubwa? Una runinga kubwa ili unitazame ndani nikipiga mitikasi yangu,” YY alijibu.

Mchekeshaji YY.
Mchekeshaji YY.
Image: Instagram//yy_comedian

Mchekeshaji YY amewaacha wengi na kicheko kikubwa baada ya kumpasha shabiki wake mmoja aliyenuia kumsimanga kwa kumiliki runinga ya kiwango kidogo hali ya kuwa yeye ni Mjaluo.

YY alikuwac amepakia video kwenye Facebook yake ikionesha vile alikuwa anafuatilia mahojiano ya wagombea wenza wa urais katika mkumbo wa kwamba ambao uliwashirikisha wagombea wa George Wajackoyah na David Mwaure, Justina Wamae na Ruth Wamae mtawalia.

Kwenye video hiyo, alikuwa ameficha picha ya mgombea mmoja kwenye uso wa runinga kwa kutumia nguo huku akimsikiliza na kumtizama mwingine huku akifuatisha kwa maneno ‘maliza deni la nchi kwa siku moja’

Na kama ilivyo kawaida ya Wakenya wengi kuwa na utabaka kuhusisha baadhi ya jamii fulani na mienendo fulani, basi Wajaluo wanajulikana sana kuwa na hulka ya kupenda kumiliki vitu vyenye thamani kubwa na vya kuvutia mno kuliko watu wengine wowote.

Dhana hiyo ndiyo ilipelekea shabiki mmoja kumshambulia YY kutokana na runinga ndogo aliyoonekana akiitazama kweney video ile.

“Mjaluo ako na runinga ya inchi 32, unatuangusha sana wewe,” shabiki huyo kwa jina Ochenge Desire alicharuka.

YY kwa utani wake alimjibu barabara Desire na kumzima kabisa kwani hakuweza tena kurudi kuendeleza vita hivyo vya majibizano ambavyo aliviotesha mwenyewe na kushindwa kuvizima.

“Hivi unajua ni kwa nini wewe una runinga kubwa? Una runinga kubwa ili unitazame ndani nikipiga mitikasi yangu,” YY alijibu.

Utani huu wenye kumaliza ugomvi kabisa uliwapata wengi kwa kicheko kikubwa huku baadhi wakimwambia mchekeshaji huyo kukoma kuwajibu watu kwani ni kawaida yao kuingilia maisha ya watu mashuhuri mitandaoni.

“Siku zote huwa hawakosi kitu cha kusema kwa njia hasi.. usiwajali,” mmoja alimshauri YY.

Mchekeshaji YY.
Mchekeshaji YY.
Image: Instagram//yy_comedian
Mchekeshaji YY.
Mchekeshaji YY.
Image: Instagram//yy_comedian