Rotimi abaguliwa kwa rangi ya ngozi kwa kutunga wimbo kwa timu ya soka Marekani

Msanii TI alikejeli kwa kusema kwamab msanii huyo ni wa kutoka nje kabisa ya Marekani na mbona apewe mchongo kama huo.

Muhtasari

• Rotimi alipewa kandarasi ya kutunga wimbo kwa timu ya Atlanta Falcons kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Msanii Rotimi aoneshwa ubaguzi wa rangi baada ya kutunga wimbo kwa timu ya michezo Marekani
Msanii Rotimi aoneshwa ubaguzi wa rangi baada ya kutunga wimbo kwa timu ya michezo Marekani
Image: instagram

Wiki jana, timu ya kandanda nchini Marekani, Atlanta Falcons ilimpa kandarasi fupi msanii Rotimi kuwatungia wimbo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa kandanda nchini humo.

Rotimi hakuangusha kweli aliingia kweney studio na kurekodi dude moja kwa jina Rise Up kuwasifia wachezaji na timu nzima ya Atlanta Falcons.

Ila hakujua kwamab hatua ya kufanay wimbo kwa ajili ya timu ya Atlanta ndio ungekuwa mwisho wake yeye kutukanwa vibaya na wasanii wengine.

Itakumbukwa msanii huyo ambaye ana asili ya Kiafrika, wazazi wake wote wanatokea Nigeria na huko Marekani wanaishi sehemu ya New Jersey.

Sasa wakaazi wa eneo la Atlanta wameteta sana kwenye mitandao ya kijamii wakisema kwamab hatua hiyo haikufaa kwani timu hiyo ingewatumia wasanii kadhaa waliopo Atlanta na si kumleta mtu kutoka jimbo tofauti.

Rapa TI amekuwa ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wamejipata katika zogo hili baada ya kuenda ‘live’ kwenye mitandao yake ya kijamii na kutamka maneno mabaya ya kudhalilisha dhidi ya Rotimi.

TI katika klipu hiyo ambayo imesambazwa pakubwa anaonekana na kusikika akimbagua Rotimi wazi wazi kwa kusema kwamba kando na kuwa si mzaliwa na mkaazi wa Atlanta, lakini pia bado haitoshi yeye ni mtu kutoka nje kabisa ya Marekani.

Matamshi ya TI yamezua ghadhabu miongoni mwa Wamarekani Weusi ambao wamemjia juu kweli kweli wengine wakimtajia misemo kwamba kweli nyani haoni kundule kwani licha ya yeye kuwa Mmarekani mweusi ambaye anafaa kuungana na Wamarekani Weusi wenzake kupigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi ya Ngozi, lakini bado ndiye anakaa mstari wa mbele kumbagua mtu mweusi kama yeye kisa kunyimwa kandarasi ya kufanay kazi na badala yake kukabidhiwa mwanamuziki huyo.

“Mbona mnampa mchongo mtu ambaye si kutoka jiji hili, si tu kutoka kwa jiji hili ila pia kabisa kutoka nje ya nchi,” TI alionekana akitapika utumbo huo.

Wengine walisema wamemsamehe TI kwa kuelewa kwamab pengine alizungumza hivyo kutokana na hasira za kunyimwa mchongo huo ila pia wengine wakasema kwamab vita dhidi ya ubaguzi wa rangi ya Ngozi haswa katika majimbo ya Marekani itakuchukua muda mrefu sana kumalizika kwani watu Weusi wenyewe wanachukiana wenyewe.