Harmonize abuni mtindo mpya, kutembea na mwavuli hadi chooni

Msanii huyo alionekana akiwa maliwatoni na mwavuli akifanya kama anajikinga na jua au mvua vile.

Muhtasari

• Je, unaamini huu ni mtindo mpya ambao msanii Harmonize amekuja nao ama ni hali ya kujikinga na jua tu?

Harmonize na mtindo mpya wa miavuli
Harmonize na mtindo mpya wa miavuli
Image: instagram

Wasanii wengi haswa kutoka Tanzania ni mafundi wa kubuni mitindo ambayo mwisho wa siku huigwa na vijana wengi ambao wanawaangalia kama watu wa kuwafunza mitindo na mambo mengine katika maisha.

Kwa mfano miaka michache iliyopita, msanii Diamond Platnumz alibuni mtindo wa kusuka nywele kiduku pamoja na kuvalia nguo kubwa kubwa zilizokaa nyepesi, mtindo ambao vijana wengi wameanza kuiga na kukumbatia uvaaji wa nguo kama hizo zinazoonekana kama kuwapwerepweta.

Wasanii hao pia walibuni mtindo mwingine wa kuanza kutembea na vibegi vidogo kama vya wanawake na ukawa ni mtindo wa kufagiliwa sana na vijana wengi.

Msanii kutoka lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize naye hajaachwa nyuma katika mitindo.

Msanii huyo katika siku za hivi karibuni ameonekana akitembea na mwavuli katika kila kino, jambo ambalo wengi wamesema ni mtindo wake mpya kabisa ambao siku si nyingi vijana wengi watauiga.

Diamond alionekana akiwa jijini London Uingereza katika choo cha haja ndogo ambapo alionekana kujikinga na mwavuli huku akijisaidia katika maliwato hayo.

Kama hiyo haitoshi, msanii huyo tena alipakia msururu wa picha akiwa anatembea na moja akiwa ameketi kwenye kiti ambapo katika zote alionekana kutotengana kabisa na mwavuli wake, huku akitangaza kwamba Ijumaa hii anatarajia kuachia ngoma mbili kwa mkupuo.

Je, unaamini huu ni mtindo mpya ambao msanii Harmonize amekuja nao ama ni hali ya kujikinga na jua tu?