King Kaka atoa simulizi ya pili kupitia wimbo jinsi alivyougua vibaya 2021

Lost kgs ka sijui nini nilikuwa nimekonda Hakuna mlango, Kifo Ilikuwa imeGonga - wimbo huo uliimba.

Muhtasari

• "Jua ukienda ndio watakupenda, ile saying ya you don’t know what you have. Haujui marafiki watakutenda,” - King Kaka aliimba kwa sehemu.

King Kaka atoasimulizi ya pili jinsi alivyougua
King Kaka atoasimulizi ya pili jinsi alivyougua
Image: Instagram

Msanii wa kurap King Kaka kwa mara nyingine tena ametoa simulizi la hali yake ya afya iliyozua hofu kwa mashabiki wake wengi mnamo mwaka 2021.

Msanii huyo ametoa kibao cha pili ambacho kinasimulia safari yake ya matibabu wakati ambapo hali yake ya afya ilikuwa tete na kufichua kuwa mkewe Nana Owiti ndiye mtu wa kipekee aliyesimama naye kitandani usiku na mchana.

Kibao hicho ambacho amemshirikisha msanii mkongwe Kidumu kinakwenda kwa jina ‘Ahsante’

Rapa huyo aliyeshinda tuzo anasimulia jinsi alilazimika kufundishwa jinsi ya kula tena kwenye njia yake ya kupona.

 “I was alone kwa bed bila cellular Even though death was calling Trust kuna nuts Zilimove kwa hii Medula Whispers kwa pena hapo nyuma ya Goli Nikaambiwa niwe na positive mind na tests ni Negative Surrounded by close friends na Relatives Nikateachiwa kudishi Kama mtoi Mchanga Wewe ushawai kuwa na nightmares mchana Lost kgs ka sijui nini nilikuwa nimekonda Hakuna mlango, Kifo Ilikuwa imeGonga.” Sehemu ya ngoma hiyo iliimba na alinukuu maneno haya kwenye Instagram yake.

Katika wimbo huo mpya, King Kaka pia anazungumzia jinsi alivyopewa siku 30 za kuondoka lakini anashukuru kwamba ni zaidi ya mwaka sasa na bado yuko hai.

“Jua ukienda ndio watakupenda, ile saying ya you don’t know what you have. Haujui marafiki watakutenda,”

Mwaka jana King Kaka alitoa kibao cha kwanza cha kusimulia safari yake ya matibabu, collabo ambayo alimshirikisha Nviiri the Storyteller kwa jina ‘Manifest’

Kwa mara kadhaa mkewe Nana Owiti amekuwa akisimulia jinsi hali ya afya ya mumewe ilimogopesha 2021 mpaka kumsogeza karibu na Mungu.

“Nitakuwa mkweli tangu King alipougua na kuponywa, nilipata mwamko wa kiroho. Nilihisi kuchanganyikiwa. Kama familia tulitikiswa sana ilipokuwa ikitokea na tulikuwa na sehemu moja tu ya kukimbilia na hiyo ilikuwa kwa Mungu!” Nana Owiti alisimulia.

Siwezi kuhesabu mara ambazo nilimpigia simu mchungaji wangu mpendwa, Pastor Njoro ili tu kuomba nami kupitia simu. Mara kadhaa ningempigia simu tu kumwambia sikuwa na nguvu tena na mume wangu alikuwa akielekea kuisha” Nana Owiti alielezea mwezi mmoja uliopita katika ujumbe mrefu wa Instagram.