Akothee asimulia jinsi wanawake wasio na waume wamekuwa wakimtumia vibaya

Alisema kuna mmoja ambaye anamlelea watoto lakini hajawahi kuja kuona watoto licha ya kumtumia mpaka nauli.

Muhtasari

• Akothee ni mama wa watoto 5 ambaye kwa sasa anachumbiana na mwanaume mzungu.

Akothee
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

,jasiriamali mbaye pia ni mwanamuziki Akothee amesimulia kupitia ujumbe mrefu kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu matukio mabaya ambayo amewahi kuwa nayo siku za nyuma na wanawake waliodai kuwa wamama wasio na waume ili kufaidika na ukarimu wake.

Alifunguka jinsi mwanamke mmoja alipiga kambi nje ya lango lake na wanawe wawili wa kiume siku nzima, wakioka kwenye jua kali kabla ya Akothee kukubali kuwaruhusu waingie.

“Jana ilikuwa wakati mgumu sana kwangu. Kuna mama mmoja alikwama getini kwangu siku nzima akiwa na watoto wake wawili. Ndiyo, mwanzoni nilikataa kufungua lango kwa sababu nimekuwa nikiumia kwa muda kwa kuwakaribisha tu watu nisiowajua nyumbani kwangu,” Akothee alisema.

Mama huyo wa watoto watano alielezea kuwa miaka miwili iliyopita alipokea watoto kutoka kwa mwanamke aliyejidai kuwa singo lakini majanga yaliyomkuta tungesubiri afute machozi ndio asimulie.

“Miaka 2 nyuma, nilichukua wasichana 3 kutoka kwa mama wasio na waume hadi shule ya sekondari, nikawapa mama zao nafasi ya kufanya kazi na kujikimu, hawa wanawake 3 walinitelekeza na wasichana wao, waliacha kazi na sitasikia tena kutoka kwao, hata hivyo watoto wao bado wako chini ya ulinzi wangu shuleni 🙊, nimekuwa nikilipa ada ya shule, wiki chache zilizopita, mama mmoja wa wasichana alinipigia simu.”

Alisema kuwa mama huyo alimtaka kutuma nauli ili aje kuwaona watoto wake lakini alipotuma mama huyo aliingia mitini hata hakupiga simu kusema kwa nini hakutokea kuwaona watoto licha ya kupokea nauli kutoka kwa Akothee.

“Kwa hivyo mimi kwa ujinga wangu, nilimtumia Leah nauli, Sijamkazia macho Leah wala kusikia kutoka kwa Leah, Leah hajamuona hata binti yake tangu miaka 2 🤣🤣 inasikitisha Ila atakuwa anawaambia kila mtu yeye ni single mother Aah Muungano wa singo mama wenye aibu. Wanawake hawa wanapaswa kunyongwa,” Akothee alilia.