Natamani kupendwa - Pritty Vishy, asema amenyanyaswa sana mtandaoni

Vishy alisema wanamitandao wanamnyanyasa kwa kuwa mnene

Muhtasari

• Kwenye Instastory zake, Vishy alisema watu wanamnyanyasa kwa kukejeli muonekano wake ambao sasa anatamani kuwa na umbo tofauti.

• "Kupitia unyanyasaji kutoka kwa watu wanaopaswa kukushikilia, kuonewa mitandaoni na kukataliwa sio rahisi," Vishy alisema.

Mwanablogu asherehekea siku yake ya kuzaliwa
Pritty Vish Mwanablogu asherehekea siku yake ya kuzaliwa
Image: Facebook

Muundaji wa maudhui, Pritty Vishy ameeleza huzuni yake ya kunyanyaswa mtandaoni na watumizi wa mitandao.

Kwenye Instastory zake, Vishy alisema watu wanamnyanyasa kwa kukejeli muonekano wake ambao sasa anatamani kuwa na umbo tofauti.

"Natamani ningekuwa na mwili mzuri ambao kila mtu ataupenda, kwa sababu ukiwa mnene kila unapoenda unanyanyaswa na kutusiwa tu," Vishy aliandika.

Alidokeza kutaka kukata tamaa iwapo unyanyasaji huo utazidi na kusema kuwa iwapo atakata tamaa basi tufahamu kuwa matendo ya wanamitandao yamemlemea.

Vishy alisema kuwa hali yake haijakuwa rahisi haswa kwa sababu hana mtu wa karibu ambaye anaweza kuongelesha.

"Kibaya zaidi ni kukosa mtu ambaye atakushika, atakupa moyo na nguvu ..Hata kukumbatiwa ili kupunguza maumivu na huzuni," alisema.

Mpenzi huyo wa mwanamuziki Simple Boy wa zamani aliwashauri watu kuwa wakarimu kwa watu wengine.

"Kupitia unyanyasaji kutoka kwa watu wanaopaswa kukushikilia, kuonewa mitandaoni na kukataliwa sio rahisi, wakati mwingine natamani kupendwa hata na wachache tu lakini nani atanipenda?" Vishy alisema.

Alieleza kuwa wanamitandao hutarajia mengi kutoka kwa watu maarufu ila hawajali hali yao ya kiakili.

Haya yamejiri baada yake kukashifiwa na wanamitandao kwa kudokeza kuwa shoga alipoonekana akimbusu mwanamke kwenye mtandao wa TikTok.

Hivi majuzi, Pritty Vishy alionekana kuhangaishwa na upweke na kuwa na kumbukumbu za maisha yake ya hapo awali.

 Vishy alikuwa mwenye huzuni kwa kuwa hana mpenzi haswa mwaka unapoelekea kuisha.

"Kwani mmeniamuliaje? Nilianza mwaka nikiwa kwenye uhusiano mzuri ila kwa sasa sina hata kamoja," Vishy aliandika huku akiongeza emoji inayolia na jicho moja.