Juliani azindua rate-card yake ya shilingi milioni moja

Rate card hiyo iko katika vipengele vitatu na alisema ana ana zaidi ya wafuasi milioni 2 mitandaoni kati ya miaka 24-35.

Muhtasari

•Vipengele vyote vina bei zinazoenda hadi mwaka mzima huku kila kimoja kikitoa maelezo ya faida zake na ni mara ngapi matangazo yatafanywa mitandaoni.

Juliani azindua rate card
Juliani azindua rate card
Image: Insgaram

Julius Owino, rapa wa Kenya almaarufu kama Juliani amekuwa msanii wa hivi punde kuzindua rate-card yake kwa wale wanaotaka kushirikiana naye kwa biashara za mitandaoni.

Rate-card hiyo ambayo ilipakiwa kwenye mtandao wa Twitter ina vipengee vitatu, kipengele cha kwanza kile cha kufaidi kwa ngazi moja ya kila mmoja kupata thamani ambacho kinaenda kwa shilingi laki mbili na nusu pesa za Kenya kwa mwaka.

Kipengele cha pili ni kile cha program jalizi ambapo kama unamtaka akupe shavu katika kazi zako za kimitandao basi unamuita kwa shilingi nusu milioni kila mwaka.

Cha tatu ambacho ni ghali zaidi kinaenda kwa shilingi milioni moja kwa mwaka ambacho ni cha kipekee kwenye mambo spesheli tu.

Katika usajili wa kipengele cha kwanza cha laki mbili unusu, unapata faida kutoka kwa rate card yake kwa punguzo la asilimia 30, matangazo yako kuwekwa kwenye mitandao yake ya kijamii mara moja kwa kila mwezi miongoni mwa faida zingine.

Image: Twitter

Kwenye kipengele cha pili, punguzo linakuja kwa asilimia 50 huku matangazo yako yakipakiwa kwenye mitandao yake mara mbili kwa mwezi.

Sawia na kitengo cha tatu cha milioni moja kwa mwaka, punguzo lipo kwa asilimia 70 huku kila mwezi matangazo ya biashara zako yakipakiwa mara nne kwa mwezi, ina maana kila wiki tangazo lako linapeperushwa na Juliani aliyesema ana zaidi ya wafuasi milioni mbili wa kati ya miaka 24 hadi 35.

Haya basi chaguo ni lako!