Massawe Japanni amsuta DJ Brownskin kumrekodi mkewe akinywa sumu, "Si hata ungepanick!"

Massawe alitilia shaka kwamba huenda hata DJ Brownskin hakumuomboleza mke wake baada ya kufa.

Muhtasari

• Hata hivyo, mtu asiwahi kukuendesha hadi kufikia hatua hii!!!!! Hakuna anayestahili kuchukua maisha yako - Massawe.

DJ Brownskin katika mazishi ya mke wake.
DJ Brownskin katika mazishi ya mke wake.
Image: Instagram

Wikendi iliyopita, mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi kulienezwa video na hadithi ya kutamausha jinsi DJ Brownskin alimrekodi mke wake akinywa sumu hadi kufa bila kuchukua hatua zozote za dharura.

Mtangazaji wa Radio Massawe Japanni ni mmoja wa watu ambao wamejitupa katika suala hilo na kutoa maoni yake kuhusu video hiyo ya kukera ambayo watu wengi wameizungumzia, baadhi wakimtetea Brownskin kwa kutonusuru maisha ya mke wake na wengine wengi wakimsuta kwa kutofanya chochote kumkanya asijiuwe.

Kulingana na Massawe, kitendo cha kutofanya chochote Zaidi ya kumrekodi na kumshangilia akikoroga, na kupiga funda la sumu ile ni upuuzi mtupu ambao haufai kutetewa kwa njia yoyote ile.

Massawe alisema kuwa kama mwanadamu wa kawaida, kitu cha kwanza ambacho DJ Brownskin angefanya ni kuingiwa na wasiwasi kuona mama ya watoto wake anajiua, jambo ambalo halikuonekana kumtisha hata kidogo.

“Uzembe mtupu!!!! Kitu cha kawaida ambacho angefanya ni kuogopa wakati anakunywa sumu mara ya kwanza, alipata nafasi nyingine ya kumuokoa alipoona anatokwa na povu! Lakini Hakushtuka hata kidogo!” Massawe alisema.

Aidha, Massawe akiuliza kama ilikuwa lazima kurekodi video ile ukilinganisha na kuokoa maisha ya mke wake.

Mtangazaji huyo alisema kuwa mtu kama DJ Brownskin hafai kupata upendo wowote katika jamii kwani hakuonesha upendo kwa mke wake, huku pia akishauri watu kutokubali kufikishwa katika hatua ya kujitoa uhai na wale wawapendao.

“Je, kulikuwa na umuhimu gani kwake kurekodi video hiyo? Maudhui ya nani???? Inasikitisha kwamba watu kama huyu hawana moyo! Dhamiri sifuri !!Nina shaka kama kweli anamwomboleza. Hata hivyo, mtu asiwahi kukuendesha hadi kufikia hatua hii!!!!! Hakuna anayestahili kuchukua maisha yako!!!! Mtu mbaya!!!” Massawe alisema.

Mke wa DJ Brownskin alizikwa mwaka jana mwezi Julai lakini video ya kuonesha jinsi alipata umauti wake ilivujishwa wikendi na BNN na imezua gumzo pevu, maoni mtanange, wengi wakionekana kumshtumu Brownskin kwa kigezo kwamba, hata kama mke wake alikuwa mbaya kiasi gani, hiyo si sababu ya kumchochea kutoa uhai wake akimshangilia bila msaada.