Ushauri wa Betty Kyallo kabla ya kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi

Betty alidai kuwa yafaa watu waangalie malengo ya mtu bali si urembo pekee

Muhtasari

• Mfanyibishara huyo anamiliki kampuni ya flairby Betty ya kutoa huduma ya urembo na bidhaa za urembo.

Image: INSTAGRAM// BETTY KYALLO

 

Mjasiriamali Betty Kyalo amewashauri kina dada kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi, mwanzo wahakikishe wamejirembesha zaidi.

Kwenye mtandao wake wa Instagram,Betty aliwapa himizo wanaume kuwa  kando na urembo alio nao msichana waangazie nidhamu ya kazi walio nayo malengo yao na ndoto zao na nyoyo zao kubwa.

"Kuwa mpenzi mrembo na hata ex mrembo zaidi," alisema.

"Sahau mwonekano wake, vipi kuhusu maadili yake ya ajabu ya kazi, matamanio yake yaziyozuilika na moyo wake mkubwa wa ajabu," aliongezea Betty.

 

Betty  ni mwanabiashara ambaye amejikuza mwenye biashara ya kuuza  bidhaa za urembo na kutoa huduma za urembo na kampuni yake ya flairby Betty. Amefungua matawi kadhaa ya kampuni hiyo likiwemo la juzi zaidi kule Meru.

Betty ni mwanamke mwenye kujiamini na kujivunia yale aliyofanikisha katika maisha.

Hivi majuzi wakati wa mahojiano na mwanasiasa maarufu Phelix Odiwuor almaarufu Jalang'o, Betty alizungumza kuhusu mapenzi na uhusiano, biashara, uhalisia, na jinsi walivyofichua kuwa kwa sasa wanafanyia kazi Kyallo Kulture msimu wa 2.

Mfanyibiashara huyo alifichua kuwa amekuwa akichumbiana kwa karibu mwaka mmoja na amekuwa akiweka uhusiano wake kuwa wa faragha kwani wakati huu anataka kufanya mambo tofauti na kuona jinsi mambo yatakavyokuwa.

Hapo awali Betty alipoulizwa ni kwanini amekuwa akihamisha biashara yake kutoka eneo moja hadi lingine, mfanyibiashara huyo mwenye umri wa miaka 34 alisema kuwa anapenda miradi mipya na anapenda kuwapa wateja wake fursa na uzoefu wa ajabu na kuongeza kuwa mabadiliko ni mara kwa mara.

Alibainisha kuwa, "Nikipata eneo si zuri kwa wateja wangu, sina tatizo la kuhama na kuongeza kuwa mabadiliko ni ya mara kwa mara ikiwa unaona kitu hakifanyi kazi, unahitaji tu kuhama na kuanza upya." Pia alisema kuwa eneo jipya ni la uboreshaji na anafurahi sana kuanza safari yake mpya.