Kumchora tattoo mwanamke si kumheshimisha - Mwijaku amkoromea Rayvanny

Mwijaku alimtaka Rayvanny kumheshimisha Fahyvanny kwa kumuoa kwenye ndoa ya kidini, kwani tayari ameshamtesa sana.

Muhtasari

• Karipio hili linakuja saa chache baada ya Rayvanny kuonesha picha akiwa amechorwa tattoo ya jina la mpenzi wake Fahyvanny kwenye mkono wake.

Mwijaku amtaka Rayvanny kukuoa fahyvanny na kuacha michezo ya kuchora tattoo.
Mwijaku amtaka Rayvanny kukuoa fahyvanny na kuacha michezo ya kuchora tattoo.
Image: Twitter//Mwijaku.

Mwijaku, mtangazaji mbwatukaji na mwenye utata na ubishi mwingi amemkaripia kwa ukali msanii Rayvanny kwa kuchora tattoo ya mpenzi wake wa muda mrefu ambaye pia ni mzazi mwenzake, Fahyvanny.

Kulingana na Mwijaku, kumchora tattoo mwanamke si kumheshimisha, akisema kuwa heshima kamili itokayo kwa mwanamume moja kwa moja kwenda kwa mwanamke ni kumuoa kabisa tena kwa ndoa ili kupata Baraka za Mungu.

Mwijaku alimkoromea Zaidi Rayvanny akidai kuwa amemmtesa Fahyvanny kwa muda mrefu, na pia kuzua cheche kuwa msanii huyo amekuwa akihanya mpaka kuambukizwa ugonjwa wa UTI.

Kumchora TATOO sio kumuheshimisha mwanamke. Muoe umpe heshima na apate baraka za Mungu. Umemtesa sana na wasambaza U.T.I sugu,” Mwijaku alisema.

Alisema kuwa mambo ya kuchora tattoo ili kumfurahisha mwanamke si ya msanii huyo bali ni ya Harmonize, akimtaka kukoma kujipendekeza.

"Kama unampenda kweli Muoe na sio utoto wa kuchorana . Hizo swaga muachie KONDE . Hakuna mnyakyusa wa aina hiyoo," Mwijaku alifoka.

Karipio hili linakuja saa chache baada ya Rayvanny kuonesha picha akiwa amechorwa tattoo ya jina la mpenzi wake Fahyvanny kwenye mkono wake.

Msanii huyo alidokeza kurudiana na Fahyvanny wiki mbili zilizopita, baada ya kumshirikisha kama vixen kwenye video ya wmbo wake wa ‘Forever’

Wapenzi hao wawili ambao walianza kuchumbiana mwaka 2015 walibarikiwa na mtoto mmoja wa kiume mwaka 2017 kabla ya kuachana mwaka 2019 kufuatia sakata la mwanamke vixen aliyeonekana kweney video ya Rayvanny ya kipindi hicho ‘I Love You’.

Baada ya kuachana Rayvanny alianza kuchumbiana na Paula, binti wa Kajala Masanja lakini pia penzi lao lilikosa ladha mwaka jana na kila mmoja kuamua kujishughulisha na hasmini za kwake.

Mwijaku sasa anadai kwamba Paula aliwaambukiza Harmonize na Rayvanny ugonjwa wa UTI huku pia akimtaadharisha Marioo, ambaye siku za hivi karibuni amedokeza kudekezana na Paula mitandaoni kuwa awe makini na binti huyo kwani anaeneza UTI kwa watu wengi.