•"Kwa mume wangu ... nilikuchagua wewe kwa wanaume wote. Imiliki na ujivunie ... usiruhusu wasiwasi wa mapenzi uharibu tulichonacho ... kwa upendo Bi Lutaaya," aliandika mke wake Shakib.
Baada ya drama zote zilizotokana na filamu ya Young, Famous and African, mwanasosholaiti wa Uganda, Zari Hassan aliandika ujumbe wa kuthibitisha upendo wake kwa mumewe mdogo, Shakib Cham Lutaaya kwenye Instastory yake.
"Kwa mume wangu ... nilikuchagua wewe kwa wanaume wote. Imiliki na ujivunie ... usiruhusu wasiwasi wa mapenzi uharibu tulichonacho ... kwa upendo Bi Lutaaya," aliandika mke wake Shakib.
Hii ni baada ya aliyekuwa mpenzi wake na mzazi mwenzake Diamond Platnumz kuibua madai kwamba bado Zari anampenda na hata alitaka kupata mtoto mwingine naye.
Siku chache zilizopita mwanasosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 42, alishtumu aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz kwa kuharibu ndoa yake.
Baadaye Zari alidokeza kuwa madai ya staa huyo wa Bongo dhidi yake yalisababisha mgogoro katika ndoa yake mpya na Shakib.
Katika tukio moja kwenye filamu ya uhalisia iliyoachiwa siku ya Ijumaa, Young, Famous and African sehemu ya pili, Diamond Platnumz alisikika akimwambia mshikaji wake mpya, Francine Koffie almaarufu Fantana kutoka Ghana kwamba mpenzi wake wa zamani Zari Hassan alitaka mtoto wa tatu naye.
Katika majibu yake yaliyojaa machungu, Zari Hassan alikanusha madai kuwa bado anampenda mwimbaji huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 32 na kwamba aliomba kuzaa naye mtoto mwingine.
Mwanasosholaiti huyo alidai kuwa Diamond ndiye amepata ugumu wa kusonga mbele baada ya. mahusiano yao kuvunjika.
Kutokana na hayo, aliweka wazi kuwa uhusiano wao hautakuwa sawa tena na kubainisha kuwa anaweza kujisimamia mwenyewe.