Hatuachani ni mapunziko tu ya muda- Sauti Sol

"Imekua safari ya kufurahisha ya miaka 15 kwenye muziki na sasa imefika wakati ambao tunahisi tunafaa kupumzika kwa muda " alisema Polycarp.

Muhtasari

• Tamasha hilo la Stanbic Yetu Festival huenda ni mara ya mwisho ambapo mashabiki wa bendi hiyo kuwaona wakitumbuiza pamoja.

• Tamasha hilo ambalo linaandaliwa kwa mara ya pili linafadhiliwa na benki ya Stanbic kwa ushirikiano na kampuni ya Radio Africa Group.

Bendi ya sauti sol.
Bendi ya sauti sol.
Image: INSTAGRAM/ SAUTI SOL

Mwanachama wa bendi ya Sauti Sol, Polycarp Otieno amesema kuwa kundi hilo halijatengana ila litachukuwa tu mapunziko ya muda.

Akizungumza na vyombo vya habari kabla ya tamasha la Stanbic Yetu Festival, Polycarp alipuuzilia mbali madai ya kuwa kundi hilo litagwanyika kabisa. 

"Imekua safari ya kufurahisha ya miaka 15 kwenye muziki na sasa imefika wakati ambao tunahisi tunafaa kupumzika kwa muda " alisema Polycarp.

Aliwahakikishia mashabiki wao kuwa kundi hilo haliwachi kufanya muziki au kugawanyika ni mapumziko tu ya muda.

"Hatuachi kufanya muziki ama kuachana, ninataka mfahamu hivyo, ni mapunziko tu madogo hakuna kitu kingine", Polycarp alisema.

Aliongeza kuwa..."Imekua safari ya kusisimua ya miaka 15 kwenye muziki pamoja na sasa umefika wakati ambao tunahisi tunafaa kupumzika kwa muda ".

Washindi hao wa tuzo ya MTV kama kundi bora la Afrika mwaka wa 2014 na 2015 walitangaza kuchukua muda wa mapumziko kila mmoja akifanya muziki kivyake. 

Tamasha hilo la Stanbic Yetu Festival huenda ikawa mara ya mwisho ambapo mashabiki wa bendi hiyo watawaona wakitumbuiza pamoja.

Kundi la Boyz II Men walisema pia wao wamewai kuchukua mapunziko kama hio hio inayochukuliwa na kundi hilo la Sauti Sol kwa kipindi cha miaka miwili na iliwaisidia katika taaluma yao ya muziki.

Bendi ya Sauti Sol ni moja wapo wa wasanii wa Kenya ambao watapata nafasi adimu ya  kupanda jukwaa moja na mastaa wa muziki kutoka Marekani la Boyz II Men watakaotumbuiza Jumamosi katika tamasha la Stanbic Yetu Festival katika bustani ya  Uhuru Gardens jijini Nairobi.

Tamasha hilo ambalo linaandaliwa kwa mara ya pili linafadhiliwa na benki ya Stanbic kwa ushirikiano na kampuni ya Radio Africa Group.