Utaishawishi aje serikali kuwa huna pesa wakati mitandaoni unajionesha wewe ni milionea?

Jalang'o ambaye pia ni mwanablogu alisema kuwa wanablogu wa mitandaoni ndio waliojiingiza katika mtego huo ambao ni vigumu kujitoa, na hivyo kuwa vigumu kuwatetea dhidi ya ushuru 15%.

Muhtasari

• Jalang'o alioneshwa video ya Mulamwah akila githeri huku kwenye sahani kukiwa na pesa na kutakiwa kumtetea kuwa kweli hana pesa, jambo ambalo alishindwa.

• Pia alionesha video ya Amber Ray akisema kuwa kwa siku yeye hutumia laki 3, na kutakiwa kummtetea kuwa hawezi kulipa ushuru wa 15%.

Jalang'o asema wanablogu ndio walijiingiza kwenye mtego na ameshindwa kuwatetea dhidi ya kutokatwa ushuru.
Jalang'o asema wanablogu ndio walijiingiza kwenye mtego na ameshindwa kuwatetea dhidi ya kutokatwa ushuru.
Image: Instagram

Mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor alaarufu Jalang’oo amesema kuwa imekuwa vigumu kuwatete wakuza maudhui na wanablogu wa mitandaoni dhidi ya pendekezo la serikali kuhusu kukatwa ushuru wa 15% kwa kile wanachokifanya mitandaoni.

Katika video ambayo mbunge huyo ambaye pia ni mkuza maudhui aliyopakia kwenye YouTube yake, alisema kuwa alikuwa jijini Kisumu katika mkutano wa kamati ya bunge kuhusu ushuru kwa wakuza maudhui.

Alisema kuwa alikuwa anajaribu kuwatetea kuwa hawana pesa za kuwawezesha kukatwa ushuru wa asilimia 15 lakini ilikuwa vigumu kidogo kwa upande wake, kwani alishindwa kuwashawishi wenzake kuwa wanablogu kweli hawana pesa.

Jalang’o alisema kuwa wanablogu hao ndio walijiingiza kwenye mtengo kwa kile alisema kuwa mitandaoni wanajigamba na kujishaua jinsi walivyo matajiri, wengine wakionesha mali ya thamani kubwa ambayo wanamiliki kutokana na kazi za kukuza maudhui, hivyo kuiaminisha serikali kuwa wana hela ndefu ambayo inafaa kukatwa ushuru wa 15%.

“Ni vipi ni nitawashawishi serikali au mtu ambaye haelewi ukuzaji maudhui kuwa hamna pesa na hamna uwezo wa kulipa ushuru wa 15% wakati kile mnachokionesha huko nje ni kwamba nyinyi ni mamilionea?” mbunge huyo aliuliza wanablogu.

Alisema kuwa ilifikia hatua ya wanakamati hao kutembelea baadhi ya akaunti za wanablogu hao wanaolia hawana hela ya kukatwa ushuru na kuona jinsi wanajitapa kuhusu maisha ya kifahari yenye hadhi ya nyota tano.

“Baadhi ya vitu ambavyo waliniuliza, kwa mfano Oga Obinna amefikisha miaka 33 na amejipatia zawadi ndogo, nah ii zawadi ndogo ni gari ambalo linaweza kumgharimu kiasi cha milioni 6 au 7. Nilisema hiyo ni mfano kidogo…. Pia wakanionesha video ya Amber Ray akisema anatumia laki 3 kwa siku… wakaendelea kunionesha kurasa za wanablogu na maisha yao ghali…” Jalang’o alisema.

 Mbunge huyo alisema kuwa ushahidi huo ulimweka katika nafasi ngumu ya kuwatetea wanablogu huo dhidi ya pingamizi ya kulipa asimilia 15 ya ushuru kwani wenyewe huwa wanajionesha kuwa wana mamilioni ya hela.