Babake Mohbad amewaomba watu msamaha kwa kuharakisha kumzika msanii huyo

Babake Mohbad alisema ni kwa sababu hawakuweza kupata nafasi katika chumba cha kuhifadhia maiti kuhifadhi mwili wake.

Muhtasari

• "Tulinyimwa taarifa ya polisi kituoni,Tulijaribu kumpeleka chumba cha kuhifadhia maiti lakini hapakuwa na nafasi, sikuweza kumtazama ndani ya nyumba," alisema.

Mohbad na babake
Mohbad na babake
Image: Screengrab

Babake msanii marehemu Mohbad, Bw Joseph Aloba, amefunguka na BBC kuhusu kifo cha mwanawe.

Katika mahojiano mapya huku kukiwa na taharuki kuhusu kifo cha mwimbaji wa Nigeria mwenye umri wa miaka 27, bwana Joseph Aloba, ameomba radhi kwa kumzika mwanawe kwa haraka.

Mohbad alifariki Jumanne, Septemba 12, 2023 na akazikwa siku iliyofuata.

Akielezea kwa nini mwimbaji huyo alizikwa haraka hivyo ingawa hakuwa Mwislamu, babake alisema ni kwa sababu hawakuweza kupata nafasi katika chumba cha kuhifadhia maiti kuhifadhi mwili wake.

“Mwanangu alikufa saa tatu usiku hakuna aliyenipigia simu.Nilipofika nyumbani kwake ilikuwa saa nne usiku nikaona watu wengi sana.Tulinyimwa taarifa ya polisi kituoni,Tulijaribu kumpeleka chumba cha kuhifadhia maiti lakini hapakuwa na nafasi, sikuweza kumtazama ndani ya nyumba," alisema.

“Akiwaomba radhi mashabiki wa mwimbaji huyo wa ‘Peace’ waliojawa na hasira alisema “Ilibidi nimzike, Wanaijeria wanisamehe nikiwakosea, hakuna anayempenda kama mimi, sijawahi kumuona Samlarry maishani mwangu, siku ya kwanza nilipoenda nyumbani kwa Naira Marley, Mohbad alikuwa anakula na Naira akachukua kijiko na alikuwa anakula naye.”

Katika mahojiano hayo yaliyofanyika kwa lugha ya Kiyoruba, aliendelea kusema "Hii ilinigusa sana kwamba alikuwa akimpenda sana lakini mwanangu aliniambia Naira ni mbaya. Nilipoenda chumbani kwa Naira ili kumsihi amsamehe mwanangu chochote ambacho angeweza kufanya, sikujua alikuwa akinirekodi".

Aliongeza kuwa “Samlarry kwa mara ya kwanza aliwahi kumpiga aliniambia nisiongee chochote, aliripoti kituo cha polisi lakini hakuna kilichofanyika, tangu wakati huo alikuwa akiishi kwa hofu, alipigwa tena wakati wa kushoot video yake na Zlatan. Nahitaji haki kwa ajili yake".

"Kama Mchungaji, siwezi kupigana na jadi kwa sababu ya dini yangu. Ikiwa wanataka kufanya uchunguzi wa DNA, waache wafanye hivyo" alihitimisha.