Edday Nderitu afurahi baada ya kutimiza ndoto ya kununua shamba kwa jina lake

" Furaha ya kumiliki kitu ambacho umetamani kwa miaka mingi inasisimua kabisa - ndoto imetimia,” Nderitu alisema.

Muhtasari

• "Rafiki yangu alinitambulisha kwa kampuni moja…Nililipa within many months mpaka nikamaliza na sasa niko na title yangu" alisema.

Edday Nderitu.
Edday Nderitu.
Image: Facebook

Edday Nderitu, mke wa msanii wa Mugithi Samidoh ni mama mwenye furaha baada ya kufanikisha ndoto yake ya muda mrefu – kuwa na kipande cha ardhi kilichosajiliwa chini ya jina lake.

Nderitu ambaye hivi majuzi kupitia ukurasa wake wa Facebook aliuliza wafuasi wake kuhusu uzoefu wa kumiliki shamba nchini, alivunja taarifa hizo njema akisema kwamba kwa muda mrefu alikuwa anatamani sana kumiliki shamba.

Nderitu alisema kwamba safari yake ya kumiliki shamba ilianza muda Fulani nyuma lakini kipindi hicho hakuwa na uwezo kwa vile hakuwa na pesa za kutosha wala kazi maalum ya kutegemewa.

Lakini baada ya rafiki yake mmoja kumuunganisha kwa dalali mmoja wa mali isiyohamishika, aliweza kupata mpango wa kulipia pole pole na hatimaye sasa amekabidhiwa hati cha kumiliki shamba.

“Wakati fulani huko nyuma, nilikuza hamu ya kumiliki kitu changu - kuwa maalum chini ya jina langu. Lakini sikuwa nimeweka akiba nyingi na sikuwa na mapato ya kawaida, kwa hivyo sikuwa na uhakika jinsi ya kuifanya. Rafiki yangu alinitambulisha kwa kampuni moja…Nililipa within many months mpaka nikamaliza na sasa niko na title yangu…yes all mine. Furaha ya kumiliki kitu ambacho umetamani kwa miaka mingi inasisimua kabisa - ndoto imetimia,” Nderitu aliandika kwa furaha.

Wakati Nderitu anafurahi kupata shamba, mpenzi wake Samidoh na mama watoto wake KarenNyamu wikendi walijumuika na wanasiasa wengine katika kaunti ya Murang’a ambapo walihudhuria hafla ya kitamaduni ya kulipa mahari iliyowahusisha mbunge wa Mathira Eric Wamumbi na Betty Maina, mwakilishi wa kike kaunti ya Munrang’a.

Licha ya kumiliki shamba nchini Kenya, Edday bado yuko nchini Marekani lakini ishara ya kununua shamba humu nchini ni idhibati tosha kwamba huenda ana ndoto ya kurejea Kenya – lakini si kwa ndoa yake bali kujitegemea katika kipande chake cha ardhi.