Zari akumbatiana na Zuchu huku Diaomond akipigana pambaja na Shakib (video)

Video ilionyesha Diamond na Shakib wakiwa ndio wameketi huku Zuchu na Zari wakiwa nyuma ya kochi kila mmoja akiwa amemshikilia mpenzi wake begani kwa harinjonjo.

Muhtasari

• Katika video nyingine, hao wanne walipiga toast kabla ya kujiunga na marafiki wa kipindi kingine cha uhalisia ambao walikuwa katika eneo moja nao.

Zari, Diamond na wapenzi wao
Zari, Diamond na wapenzi wao
Image: Instagram

Msanii Diamond anazidi kuwaonesha mashabiki wake mitandaoni jinsi anavyoweza kuongoza wapenzi wake wote bila tashtiti.

Wakati akiwa nchini Afrika Kusini na mpenzi wake wa sasa, Zuchu, wawili hao walipata nafasi murwa ya kukutana na aliyekuwa mpenzi na mzazi mwenza na Diamond, Zari Hassan ambapo pia naye aliwakutanisha na kipenzi chake, Shakib Cham Lutaaya.

Video hiyo ambayo imeenezwa mitandaoni, inawaonesha wanne hao wakiwa wametebwereka kwenye kochi, Diamond na Shakib wakiwa ndio wameketi huku Zuchu na Zari wakiwa nyuma ya kochi kila mmoja akiwa amemshikilia mpenzi wake begani kwa harinjonjo.

Katika video hizo, ambazo zinaonekana kuwa sehemu ya kipindi cha uhalisia cha Young, Famous, & African, ex na wenzi wao wote walikuwa na furaha walipokuwa wakikutana kwa mara ya kwanza.

Katika moja ya video hizo Zari na Zuchu walipiga soga na kukumbatiana huku Diamond na Shakib wakiwa wamekaa kwenye kochi laini wakifurahia mazungumzo ya kiume.

Katika video nyingine, hao wanne walipiga toast kabla ya kujiunga na marafiki wa kipindi kingine cha uhalisia ambao walikuwa katika eneo moja nao.

"Blended family ❤️," Zari alinukuu moja ya video hizo.

Zari ni babymama wa Diamond na walijaaliwa watoto wawili – msichana na mvulana – kabla ya ndoa yao kubuma mwaka 2018.

Tanu kipindi hicho, kila mmoja amekuwa akijaribu mahusiano ya kimapenzi kwa Zaidi ya mara moja, Zari akionekana na wanaume wawili kabla ya Shakib naye Diamond akiwa katika mahusiano ya Tanasha Donna kabla ya Zuchu.