Wanaosema Diamond ni kicheche, acha anichezee huu mwili ni wake - Zuchu

“Eti wanasema Simba ni kicheche, acha anichezee huu mwili ni wake,” Zuchu aliimba mashabiki wakimshangilia.

Muhtasari

• “Eti wanasema Simba ni kicheche, acha anichezee huu mwili ni wake,” Zuchu aliimba mashabiki wakimshangilia.

Diamond na Zuchu
Diamond na Zuchu
Image: Screegrab

Diamond na Zuchu wameendeleza onyesho lao la kumwagiana mapenzi hadharani, safari hii katika tamasha la Wasafi Festvial jijini Dodoma.

Kama kawaida yao, wawili hao waliingia jukwaani na kuimba moja ya kolabo yao – Mtasubiri sana – ambapo Diaond baada ya kuimba muda mfupi kama wamesimama, alisogea karibu na ukingo wa jukwaa na kuketi kabla ya kumuita Zuchu.

Zuchu aliitikia wito na kuketi kwenye paja la Diamond na wote wakaendeleza kuimbiana wimbo wao kwa sauti za kimahaba huku mashabiki wakiwashangilia.

Zuchu kwa ufundi mkubwa aliingiza maneno yake kwenye baadhi ya mishororo na kuonekana kutupa kijembe kwa baadhi ya watu wanaohisi kwamba Diamond hawezi kumuoa Zaidi ya kumtumia tu kimwili na baadae kumuacha – kama ambavyo amekuwa akifanya na warembo wengine aliokuwa nao katika mahusiano ya kimapenzi.

Katika hali ya kuwazima wambeya, Zuchu alisema kwamba wanaojaribu kumuasa kuachana na Dianond hawatofaulu kwani hata wakihisi anamchezea basi ni sawa sababu mwili ni wake.

“Eti wanasema Simba ni kicheche, acha anichezee huu mwili ni wake,” Zuchu aliimba mashabiki wakimshangilia na wengine kwa sauti za mbali wakisikika kusema kwamba Diamond atamuacha tu Zuchu kama alivyofanya kwenye wanawake wengine.

Si mara ya kwanza kwa wasanii hao wa WCB kuoneshana mapenzi hadharani haswa kwenye tamasha la Wasafi ambalo limekuwa likifanyika katika maeneo mbali mbali nchini Tanzania tangu mwezi Agosti.

Hata hivyo, wapo wengine ambao bado wanahisi Diamond na Zuchu hawana uhusiano wa mapenzi Zaidi tu ya mtu na bosi wake, licha ya kwamba wanalishana denda hadharani.