'Mimi sio shoga!' Nuru Okanga ajitetea picha akiwa amemkumbatia mzungu kiunoni ikisambaa

Hata hivyo, baadhi waizidi kumsakama wakisema kwamba kudai ameoa haina maana kwamba hawezi jihusisha katika suala la penzi la jinsia moja, suala ambalo Okanga amesimama kidete na kukanusha.

Muhtasari

• “Acha kuniita shoga! Yule rafiki wangu mzungu ameoa na mimi pia nimeoa,” alisema.

Nuru vOkamga na rafikiye mzungu.
Nuru vOkamga na rafikiye mzungu.
Image: Facebook

Mwanasiasa chipukizi ambaye pia ni mtetezi mkali wa sera za kiongozi wa ODM Raila Odinga, Nuru Okanga katika kipindi cha siku mbili sasa amekuwa akizua mjadalac pevu katika mtandao wa Facebook baada ya kupakia picha akiwa amekumbatiana na mwanamume mwenza mzungu.

Okanga ambaye alipakia picha hiyo juzi na kudai kwamba mzungu huyo ni wa kutokea Uholanzi ambaye alikuja nchini Kenya kwa lengo la kukutana naye kwa sababu ni shabiki wake, lakini Wakenya wanaitafsiri kivingine kutokana na jinsi wawili hao walikuwa wameshikana kwa ajili ya kupigwa picha.

Wengi katika kipengele cha kutoa maoni waliweza kumtupia Okanga kashfa ainati, wakihisi kwamba mwanasiasa huyo anayelenga kuwa MCA katika uchaguzi uchao ni shoga.

Hata hivyo, Okanga amerudi tena katika mtandao huo na safari hii amepakia picha nyingine inayomuonesha akiwa miongoni mwa watu wengine wawili pamoja na mzungu huyo na kupuuzilia mbali dai la kuwa shoga.

Okanga alijitetea vikali akisema kwamba yeye si shoga kwani mzungu huyo ni baba wa familia ambaye ameoa, lakini pia yeye ameoa kwa hivyo uvumi wa kuwahusisha na ushoga hauna mashiko hata kidogo.

“Acha kuniita shoga! Yule rafiki wangu mzungu ameoa na mimi pia nimeoa,” alisema.

Hata hivyo, watu katika maoni bado wengi walionekana kusisitiza kauli ya ushoga kwa wawili hao, wakisema kwamba anajaribu kutafuta kisingizio cha kuwapotosha.

“Kuwa katika ndoa 😂    😂sio leseni ya kuifunga Sim 2 😁 😂 😂 Wanamtandao walisema hivyo juu ya vile unamshika shika......hungemsalimia kwa njia ya KUSHIKA KWA HANDSHAKE...Funga virago mwende Majuuu anakaa Brathake Papa,” MJ TheClerk alimjulisha.

“Kwa hii picha naona tu kila mtu na mpenzi wake. Aki wewe Papa Francis” Felicis Marshall.

“Nani alikudanganya kama umeoa huwezi kufunua maboot?😂 ogopa wanaume weupe bn” One Goden Bouy.