Fahamu kile unachohitaji kufanya ili kupata kolabo na Alikiba (video)

“Inatakiwa mtu ajitafute kwanza ili usiwape watu question mark, ili angalau watu waone uwezo wako ni kiasi Fulani,” King Kiba aliongeza.

Muhtasari

• Bosi huyo wa lebo ya Kings Music alifichua kwamba hata wasanii wa lebo yake huwa anawabania vikali akiwataka kujitafuta na kujiongeza kwanza kabla ya kufanya koabo naye.

Alikiba
Alikiba
Image: Facebook

Alikiba, msanii anayetajwa na washikadau wa tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kama muimbaji bora amefunguka kwa mapana na marefu kile ambacho msanii yeyete haswa chipukizi anayetaka kufanya kolabo na yeye anahitaji kujihami nacho kabla ya kumtafuta.

Katika mahojiano ambayo aliulizwa utaratibu ukoje kuhusu msanii kumtafuta kufanya kolabo na yeye, Alikiba alisema kwamba huwa hakubali kufanya kolabo na msanii yeyote kwani kuna baadhi ya vitu ambavyo sharti msanii husika avitimize kabla ya kukubaliana kuingia mstudioni kurekodi.

Bosi huyo wa lebo ya Kings Music alifichua kwamba hata wasanii wa lebo yake huwa anawabania vikali akiwataka kujitafuta na kujiongeza kwanza kabla ya kufanya koabo naye.

Alisema kufanya hivyo ni kuhakikisha kwamba hakuna msanii anayekuja kuteleza kwa ganda la ndizi kushusha kitonga.

“Wasanii wangu mimi nimeshawahi kuwapiga mkwara siku moja, niliwaambia unataka kufanya na mimi wimbo, jitafute kwanza, kwa hiyo wapo wanaojitafuta wakijipata ndio wanakuja kufanya wimbo na mimi, watu wakishaelewa uwezo wao uko wapi. Naamini hiyo ndio njia nzuri ya kufanya kazi na mtu mkubwa,” Alikiba alisema.

Msanii huyo akijitolea mfano, alisema hata yeye leo hii akitaka kufanya kolabo na Jay Z kutoka Marekani lazima kwanza ajitafute ili ajulikane Zaidi kabla ya kumshawishi Jay Z kukubali ombi lake la kolabo.

“Kwa mfano mimi hapa nikasema nifanye wimbo na Jay Z, kuna watu watanishangaa huyu ni wa wapi kwa sababu niko na uhakika sijulikani duniani kote, unanielewa? Kwa hiyo lazima nijitafute sana tu mpaka Jay Z asikie kwamba kuna mtu, ndio hata nikifanya naye ina make sense.”

“Inatakiwa mtu ajitafute kwanza ili usiwape watu question mark, ili angalau watu waone uwezo wako ni kiasi Fulani,” King Kiba aliongeza.