Fahamu kwa nini wanawe Bahati na Diana Marua wameacha kula chips-kuku na soda

“Unajua mimi mama, hii ndio mara yangu ya mwisho ninakuja chakula cha aina hii, sitokula tena" Heaven alimpa hakikisho ama yake.

Muhtasari

• “Unajua mimi mama, hii ndio mara yangu ya mwisho ninakuja chakula cha aina hii, sitokula tena" Heaven alimpa hakikisho ama yake.

Wanawe Bahati na Diana
Wanawe Bahati na Diana
Image: Instagram

Wanawe Bahati Kioko na Diana Marua wameweka nadhiri na mama yao kwamba hawatoendelea tena kula vyakula vya haraka kama vile chips-kuku na soda.

Katika video ambayo ilipakiwa kwenye kurasa za Heaven na Majesty Bahati, watoto hao walionekana wakiwa wameketi kwenye meza kila mmoja akisasambura chips-kuku na soda kwa usanjari.

Mama yao, Diana Marua alikaribia kwenye msosi wao na kuwaasa kuweka mwisho wa kupenda kula vyakula vya aina hiyo, huku akiwakumbusha athari za vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi kwenye afya zao wangali bado wachanga.

Watoto hao wawili walikubaliana na mama yao, na binti Heaven alikula yamini mbele ya mama yake kwamba hiyo ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kula chips-kuku na soda.

“Unajua mimi mama, hii ndio mara yangu ya mwisho ninakuja chakula cha aina hii, sitokula tena, kwa sababu uliniambia nikiendelea kula nitakuwa mnono,” Heaven alisema huku kakake Majesty pia akikubaliana naye.

“Mummy anajaribu kutufundisha kwamba takataka nyingi na sukari ni mbaya kwa afya yetu ya baadaye. Tunaelewa lakini, mtu anamwambia Mama kwamba hii ni mara ya mwisho tunakula vibaya,” ujumbe kwenye chapisho hilo ulisoma.

Tazama video hiyo hapa watoto wa Bahati na Diana wakila yamini ya kutokula vyakula vya aina hiyo tena;