Diana Marua akiri kumfanana mrembo wa Nigeria aliyekutana naye mitandaoni

Mrembo huyo alikuwa amevalia kofia nyeusi na blausi ya samawati na kilichowavutia wengi kwa umakijni ni tabasamu lake ambalo kwa asilimia karibia yote linalandana na la Diana Marua.

Muhtasari

• Hata hivyo, licha ya kumtag Qing Madi, mrembo huyo wa Nigeria mpaka tulipokuwa tunachapisha habari hii hakuwa amejibu katika chapisho hilo.

Qing Madi na Diana Marua
Qing Madi na Diana Marua
Image: Instagram

Msanii wa rap ambaye pia ni YouTuber nchini, Diana Marua amepeleka katika mtandao wa Instagram kuonyesha kushangazwa kwake baada ya kukutana ghafla na video ya msanii chipukizi wa Afrobeats kutoka Nigeria ambaye anadaiwa kumfanana.

Marua alichapisha video ya mrembo huyo akizungumza na chini yake akaweka video yake na kudai kwamba watu wengi wamekuwa wkaimwambia wanafanana sana kama riale kwa ya pili.

Kwa upekuzi wa kina, ilibainika kwamba mrembo huyo wa Nigeria pia ni msanii kwa jina Qing Madi, na hakika kwa ukaribu wote ni kama dada wa toka nitoke.

Hata hivyo, Diana Marua alikanusha kumjua wala kuwahi kukutana na msanii huyo wa Nigeria, huku akiwauliza mashabiki wake iwapo ni kweli wanafanana japo mwenyewe alikiri kwamba alishangazwa kujiona katika sura ya Madi.

“Wait A Minute!!!! Nilikuwa ninajiandaa kwa ajili ya Hello Mr Right kidogo Kila mtu alikuwa kama… "Dee una pacha. Yoooo!!!! Nilikuwa kama Subiri, Nini??? Wenzangu, Je, Qing Madi kutoka Nigeria anafanana na Diana B? Kusema kweli, hapa ninakubali, kutoka upande,” aliongeza.

Aliendelea na kuwauliza mashabiki wake nini mawazo yao na watu wengi waliotoa maoni walikubaliana naye.

Hata hivyo, licha ya kumtag Qing Madi, mrembo huyo wa Nigeria mpaka tulipokuwa tunachapisha habari hii hakuwa amejibu katika chapisho hilo.

Kwa kuangalia video hii ya wote wawili, je, ni kweli wana mfanano?