Kelechi Africana ataja sababu zinazofanya Sanaa ya muziki kutoka Pwani kudorora

"Ni Wazi kwamba uandishi wenu umepitwa na wakati. Nyinyi na management zenu mnapoteza muda tu,” alisema.

Muhtasari

• Ni Wazi kwamba uandishi wenu umepitwa na wakati. Nyinyi na management zenu mnapoteza muda tu,” alisema.

KELECHI AFRICANA
KELECHI AFRICANA
Image: FACEBOOK

Klelechi Africana, mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka Pwani ya Kenya amewashambulia wasanii wenza kutoka eneo hilo kwa kile anadai kwamba wao ndio chanzo cha kutofanya vizuri kwa Sanaa ya muziki wa Pwani.

Jumatatu mchana, Africana alisema kwamba wasanii wa Pwani wengi wao ni wenye fikira finyu wasiojua wanachokifanya kwenye Sanaa.

Alisema kwamba wachache ndio wanajuana na wanasiasa wachache wanaolamba zabuni katika miradi mbalimbali lakini akasisitiza kwamba wengi wao ni vibaraka na wachache ndio wanaojua wanachokifanya kwenye Sanaa.

“Sekta ya Sanaa ya Pwani imejaa watu wenye akili ndogo ambao wanajua wanasiasa wachache ambao hupokea zabuni nyingi za bei ...Wengi ni vibaraka na ni wachache tu wanajua wanachofanya…” Kelechi Africana alisema.

 

 

Mwimbaji mashuhuri wa Mombasa anayeishi Nairobi Kelechi Africana kwa mara nyingine tena ameanzisha mashambulizi makali dhidi ya wasanii wenzake wa Pwani.

Kupitia chapisho lake, Kelechi alisisitiza kuwa wasanii wengi wa Pwani ni watu wenye akili ndogo ambao hawawezi kufikiria mikakati mikubwa ya kuinua tasnia ya muziki kwenda juu.

Katika siku za hivi karibuni, mkali huyo wa ‘Ring’ amekuwa akiendeleza mashambulizi dhidi ya wasanii wenza kutoka ukanda wa Pwani akisema kwamba wamezembea kimuziki.

Juzi-kati, Kelechi Africana alidai kwamba uandishi wa kimuziki wa wasanii kama vile Dazlah na Dogo Richy umepitwa na wakati akisema tangu wasainiwe kwenye lebo wamekuwa wakimya kwenye kuachia miziki.

Dogo Richy na Dazlah kutoka wa signiwe hawaja toa hit song …hivi nyinyi management zenu mumeshindwa kutulia mkatengeza hit song ama??? kwani mnąfeli wapi??? Ni Wazi kwamba uandishi wenu umepitwa na wakati. Nyinyi na management zenu mnapoteza muda tu,” alisema.

Vita vya maneno baina ya wasanii kutoka Pwani vimeongezeka katika siku za hivi karibuni kutokana na mtumizi mmoja mweye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii kutoka eneo hilo kunukuliwa akisema kwamba kwa sasa Pwani nzima haina msanii hata mmoja anayeweza kujaza umati wa mashabiki kwenye shoo ya klabuni huko Mombasa.