Nashukuru Mungu kwa Instagram sababu hapo ndipo nilipata mume wangu – Lucy Natasha

"Aliniandikia ujumbe DM kwa miaka 2 kama sijajibu. Alikuja na zile lines za kuniombea na kunitakia safari njema kila ninaposafiri, akiniambia ninaonekana vizuri niendelee kung’aa…" Natasha alisema.

Muhtasari

• Mchungaji huyo alifichua kwamba ni kupitia mitandao ya kijamii, haswa Instagram ambapo alipatana kwa mara ya kwanza kabisa na mume wake wa sasa Mhindi Stanley Carmel.

• Natasha alisema amekuwa katika mapenzi na nabii Carmel kwa kipindi cha miaka 2 sasa na mapenzi yao yanazidi kukomaa kila kukicha.

Lucy Natasha na mumewe Stanley Carmel
Lucy Natasha na mumewe Stanley Carmel
Image: Instagram

Mchungaji wa kanisa la ECC jijini Nairobi, Lucy Natasha amemshukuru Mungu kwa uwepo wa mitandao ya kijamii wakati wa kizazi chake.

Natasha alisema kwamba pasi na uwepo wa mitandao ya kijamii, pengine sasa hivi asingekuwa na mume.

Mchungaji huyo alifichua kwamba ni kupitia mitandao ya kijamii, haswa Instagram ambapo alipatana kwa mara ya kwanza kabisa na mume wake wa sasa Mhindi Stanley Carmel.

Natasha alisema amekuwa katika mapenzi na nabii Carmel kwa kipindi cha miaka 2 sasa na mapenzi yao yanazidi kukomaa kila kukicha.

“Kila hadithi ya mapenzi ni ya ajabu na wakati mwingine Mungu anaweza kutumia njia zozote za ajabu kuunganisha watu. Hata kwa wasio na wapenzi nataka wajue kwamba hakuna sehemu maalum ambayo unaweza ukapatana na mwenzi wako,” Natasha alianza.

“Unaweza ukapatana na mpenzi wako mtarajiwa kwa njia za ajabu kabisa, na kwetu sisi, ninamshukuru Mungu kwa uwepo wa mitandao ya kijamii kwa sababu hapo ndipo tulipokutana kwa mara ya kwanza kabisa. Instagram. Aliingia kwa DM,” Natasha aliongeza.

Alielezea jinsi walikuja kujuana na kukutana kabla ya kuwa wapenzi na muda mfupi baadae kufunga ndoa miaka miwili iliyopita.

“Kilichotokea, kumbuka hakuwa amewahi fika barani Afrika na mimi sikuwa nimefika India, aliniandikia ujumbe DM kwa miaka 2 kama sijajibu. Alikuja na zile lines za kuniombea na kunitakia safari njema kila ninaposafiri, akiniambia ninaonekana vizuri niendelee kung’aa…lakini ilinichukua muda mrefu kuona jumbe zake kwa sababu kuna watu wengi wananifollow.”

“Baadae sasa akaja kuona klipu Fulani nilikuwa nahubiri kuhusu familia ya kifalme akaja kwenye Instagram na kunifollow na kutoka hapo akaendelea kuniandikia jumbe, “endelea kung’aa”, “endelea kupeleka watu kwa Mungu”… lakini hakuwahi andika ujumbe kwamba “nakupenda”. Na baada ya miaka 2 ndio nilikuja kuona DM zake na nikasema acha nimuangalie huyu ni nani halafu nikamjibu, kama vile nilianzisha mazungumzo,” Natasha alieleza.

Baada ya hapo, Natasha alisema kuwa walikuja kukutana nchini Marekani, jimbo la Texas ambapo kila mmoja alikuwa amealikwa kivyake kwa mikutano tofauti ya injii.